Mratibu wa mafunzo (Supervisor Learning And Development) wa Barrick Tanzania, Elly Shimbi akiongea na Wanafunzi wa Vyuo vikuu wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo wa kuhimili ushindani wa ajira na kujiajiri lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC) lililofanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa udhamini wa kampuni ya Barrick.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Barrick nchini, imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuibua na kukuza vipaji vya vijana wasomi wa vyuo vya elimu ya juu na kati nchini ili waweze kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea kutokea duniani na kuhimili ushindani katika soko la ajira sambamba na kuweza kujiamini kutumia ujuzi na taaluma zao kujiajiri kwa ajili ya kujenga mustakabali endelevu.

Hayo yameeleza na Mratibu wa mafunzo (Supervisor Learning And Development) wa Barrick Tanzania, Elly Shimbi akiongea na Wanafunzi wa Vyuo vikuu wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo wa kuhimili ushindani wa ajira na kujiajiri lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC) lililofanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kampasi ya Mlimani kwa udhamini wa Barrick ambayo inaendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals.

Shimbi, pia aliwaeleza wasomi hao shughuli za kampuni ya Barrick nchini na mkakati wake wa kuinua vipaji vya vijana sambamba na kuwezesha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi ili wapate fursa ya kupata ajira katika sekta ya madini ambayo kwa sasa asilimia kubwa inatawaliwa na wanaume.

Kongamano hilo kubwa limehusisha makampuni mengine makubwa ya ndani na nje kwa ajili ya kuwanoa wanafunzi kuhusiana na mabadiliko ya teknolojia,ajira na kujiajiri wenyewe pindi wamalizapo masomo yao.
Wanafunzi wakifuatilia mada kutoka kwa Watendaji wa makampuni mbalimbali walioshiriki katika kongamano hilo.
Afisa Raslimali wa Barrick Tanzania, Isentruda Mkumba (kushoto) akiongea na wanafunzi waliotembelea banda la maonesho la Barrick kwenye kongamano hilo.
Mratibu wa mafunzo (Supervisor Learning And Development) wa Barrick Tanzania, Elly Shimbi akiwa na viongozi wa AIESEC.
Washiriki wakifanya mazoezi ya kujiweka sawa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: