WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza na kutoa mkono wa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kwa kufiwa na Baba yake Mzazi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi,alipofika Ikulu Migombani Wilaya ya Mjini Uguja Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuhani na kutowa pole kwa familia, aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa kijiji kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariamn Mwinyi, alipofika Ikulu Migombani Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole, kufuatia Kifo cha Baba Mzazi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa Kijiji kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa alipofika Ikulu Migombani kwa ajili ya kutoa mkono wa pole na kuhani Msiba wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa Kijiji kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, baada ya kumaliza kutoa mkono wa pole kufuatila kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Hayati Ahajj Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa Kijijini kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: