Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa RasilimaliWatu wa Halmashauri, Bw. David Rwazo akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiimba wimbo wa Msikamano kabla ya kuanza mkutano wa Baraza.
Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Mathew Kayanda akiwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya mwaka 2024/20245 wakati wa Baraza la Wafanyakazi wa halmashauri hiyo.
Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi TALWGU Bw.Budugu Kasuka akichangia wakati wa majadiliano ya mpango na bajeti ya mwaka 2024/2025.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mpango na bajeti ya 2024/2025.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt. Nuru Yunge akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Halmshauri ya Wilaya ya Sinyanga wamepokea, kupitia na kujadili mapendekezo yampango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Mkutano wa Baraza hilo umefanyika leo Februari, 2024 katika wa ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya wafanyakazi vikiwemo CWT,TUGHE, TALWGU , Divisheni na Vitengo vya Halmashauri.

Akifungua mkutano huo, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa RasilimaliWatu wa Halmashauri, Bw. David Rwazo amewaeleza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kuwa Halmashauri imeimarisha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi kwa kupandisha madaraja kwa wakati, kulipa madeni na kununua vitendaji kazi.

Pamoja na kupitia mapendekezo ya bajeti, wajumbe hao wamepokea na kupitia utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 na utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka kwa Mwezi Julai hadi Disemba, 2023.

Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa Bw. Mathias Balele ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sinyanga kwa jitihada inazozifanya katika kuhakikisha kuwa watumishi wake wanafanya kazi katika mazingira rafiki.

Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi hufanyika kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa Umma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: