Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid amewaasa wana CCM kutokuwa na makundi ambayo yataweza kuwagawa wanachama wake bali washirikiane kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla hasa katika kipindi hiki chakuelekea uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Mhe. Zuber ambaye pia ni Mlezi wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara katika maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM ambayo kimkoa yamefanyika katika Kijiji cha Loiborsoit A kilichopo Katika Kata ya Emboret wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

"Niwaombe wana-CCM mshikamane na muondoe makundi ambayo yanaweza kuwagawa na msiweze kushiriki vyama katika uchaguzi kuanzia wa serikali za mitaa mpaka uchaguzi Mkuu 2025," amesema Mhe. Zuber.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amesema kuwa, ndani ya kipindi kifupi mkoa wa Manyara umepokea zaidi ya bilioni 500 ambazo zimeelekezwa katika miradi mbalimbali mkoani humo ikiwemo Afya, Elimu, Maji na miundombinu, huku fedha zingine zikielekwa katika vijana, Wanawake na Walemavu kupitia mikopo ya asilimia kumi (10%) ya Mapato ya ndani.

Maadhimisho hayo yaliyobeba kaulimbiu “Miaka 47 ya CCM, Shiriki Uchaguzi kiuadilifu na Kazi iendelee” yameambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo upandaji miti katika Ofisi ya CCM kata ya Emboret, ukataji wa keki pamoja na utoaji wa zawadi kwa washindi wa kwanza na wa pili wa michezo mbalimbali
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: