Mkuu Mkoa wa Manyara Mhe Queen Sendiga ameongoza zoezi la Ugawaji wa misaada kwa kundi la wafanyabiashara wa Soko Kuu Katesh na wa mazao mbali mbali waliothirika na Maporomoko ya Matope yaliyotokea Desemba 03, 2023 na kuharibu mali zao pamoja na eneo lote la biashara hiyo.
Akikabidhi misaada hiyo kwa wahusika Mhe Sendiga ameanza kwa amewapa pole wafanyabiashara hao na kuwahakikishia kuwa serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Samia itaendelea kuwa pamoja nao kwa kila hatua mpaka pale hali itakapotengamaa kabisa.
"Rais Samia ametuelekeza tena tuje tuwaguse ninyi wafanyabiashara wa sokoni pamoja na wale wa mazao ili tuwape chakula kitakachosaidia kupunguza makali ya changamoto zilizojitokeza" aisema Mhe Sendiga
Aidha itakumbukwa kwamba misaada hii kwa kundi la wafanyabishara inakuja baada ya kukamilika kwa Misaada ya Awamu ya kwanza iliyolenga kuwasaidia waathirika waliopoteza kila kitu ikiwemo nyumba zao, ndugu zao na hata chakula chao pia.
Misaada iliyotolewa kwa kundi hili kwa kila mtu ni pamoja na; Mahindi, Mchele, Maharage, Sukari, nk
Kwa upande wake mfanyabiasha wa Soko Kuu Katesh Maria Royo ameishukuru serikali kwa misaada hiyo ambayo itakwenda kupunguza adha wanayoipata mara baada ya kupoteza sehemu ya mali zao na maeneo yao ya kufanyia biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments: