Na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG, Manyara

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga mapema leo Januari 23, 2024 amefanya ziara ya kukagua baadhi ya miradi inayoendelea katika mkoa wake wilayani Babati.

Ziara hiyo ilianzia katika Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharula (EMD) katika Hospitali ya Mji wa Babati, ambapo amewataka wasimamizi wa mradi huo akiwemo mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kujitahidi ujenzi wa jengo hilo unakamilika kwa haraka.

Akitoa taarifa Mganga Mkuu wa Mji Daktari Kyabaroti Kyabaroti amesema kuwa jengo hilo lilitengewa Mil. 300 ambapo mpaka sasa lipo katika hatua za umaliziaji na ifikapo mwanzoni mwa mwezi wa Februari litaanza kutumika.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga akiteta jambo na Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara ililopo eneo la Maisaka Katani kata ya Maisaka, Babati Mjini.
Pia, Mhe. Queen Sendiga alipata wasaa wa kutembelea ujenzi wa jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara ililopo eneo la Maisaka Katani kata ya Maisaka, Babati Mjini ulioanza Oktoba 25, 2023.

Mhe. Sendiga amejionea ujenzi huo huku akiwataka wataalamu hao kumaliza kwa wakati bila kutoa visingizio vyovyote vitavyosababisha ukwamishaji wa ujenzi huo.

Ujenzi huo unaogharimu shilingi Mil. 600 ambapo awamu ya kwanza wamepewa zaidi ya mil. 285 kwa ajili ya ukamilishaji wa Boma, msingi mpaka gorofa ya kwanza na sasa ujenzi umefikia asilimia 21.4.

Aidha Jeshi la Zimamoto Walimemshukuru Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuendelea kuwezesha majeshi ya Tanzania katika kukabiliana na majanga mbali mbali huku wakimshukuru Mhe. Sendiga na ofisi yake kwa ujumla kuweza kuwawezesha katika miongozo mbali mbali.
Mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara linalojengwa eneo la mkoani wilayani Babati. 
Baadae Mhe. Queen Sendiga alifika katika mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara linalojengwa eneo la mkoani wilayani Babati. Mradi ulibuliwa baada ya Serikali kuanzisha mkoa wa Manyara mwaka 2002 na ndipo uhitaji wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa ulipotokea.

Jengo hilo la ghorafa nne ambapo likikamilika litakuwa na jumla ya vyumba vya ofisi 33 kati ya hivyo 06 ni vyumba vya ofisi za maafisa wakuu ngazi ya mkoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amesema utekelezaji unaoendelea ni awamu ya Kwanza ambayo ilianza baada ya Serikali kutoa fedha mnamo mwezi Aprili 2023 jumla ya shilingi milioni mia nane tu (TShs.800,000,000.00) ambazo zilipokelewa Polisi Mkoa Manyara.

Amesema kazi zilizofanyika ni ujenzi wa msingi, nguzo na sakafu za ghorofa zote nne huku wakifanya maandalizi ya ujenzi wa kuta za pamoja na kuezeka na ujenzi wa chumba cha mitambo ya lifti ambapo wanatarajia ujenzi huo ukamilike mwishoni mwa mwezi Februari.

Nae Mhe. Sendiga amewapongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kwa kutekeleza mradi kwa vitendo huku akizitaka taasisi nyingine zenye miradi mkoani humo kuiga Jeshi la Polisi.

Aidha Mhe. Sendiga amemtaka mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kuhakikisha anasimamia kwa ufasaha ujenzi wa jengo la ofisi ya yake linakamilika kwa wakati maana ujenzi wake umekuwa ukisua sua jambo linaloleta ukakasi kila anapotembelea.

Jengo la ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Babati ambapo ujenzi wake umekuwa ukisua sua. (Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG, Manyara)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: