Mkufunzi wa kutumia mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) kutoka nchini Afrika Kusini Linda Veale akiwafundisha wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) (hawapo pichani) namna ambavyo mashine hiyo inavyoweza kufanya uchunguzi na vipimo mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mafunzo ya namna ya kutumia mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) wakati wa mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijifunza kwa vitendo namna ya kuunganisha vifaa vya kumuunganisha mgonjwa na mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa kutumia mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) kutoka nchini Afrika Kusini Linda Veale akiwaonesha wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) namna ambavyo mashine hiyo inavyofanya kazi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Picha na: JKCI
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: