Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (Mb), akipokea Salaam ya heshima kutoka Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji asubuhi ya leo Februari 26, 2021 katika uzinduzi wa ushirikiano wa programu ya mafunzo kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Chama cha Skauti Tanzania Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji Dodoma.
Gwaride maalum la heshima la askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likitoa salamu ya heshima kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo, Mb (Hayupo pichani) asubuhi ya leo Februari 26, 2021 alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuzindua ushirikiano wa programu ya mafunzo kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Chama cha Skauti Tanzania
Msemaji wa Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja akielezea matumizi ya vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na askari wa Zimamoto na Uokoaji wakati wa maokozi kwa Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, Mb (Kushoto) leo tarehe 26 Februari, 2021 katika uzinduzi wa ushirikiano wa programu ya mafunzo kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Chama cha Skauti Tanzania Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (Mb), akizungumza na washiriki wa uzinduzi (Hawapo pichani) wa ushirikiano wa programu ya mafunzo kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Chama cha Skauti Tanzania leo tarehe 26 Februari, 2021 Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, Mb (Wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja ya uzinduzi wa ushirikiano wa programu ya mafunzo kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Chama cha Skauti Tanzania. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Khamis Hamza Chilo (Mb), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF John Masunga (Wa pili kushoto) na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Bi. Mwantumu Mahiza (Kulia).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, Mb (Wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, leo tarehe 26 Februari, 2021 katika uzinduzi wa ushirikiano wa programu ya mafunzo kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Chama cha Skauti Tanzania Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, Mb (Wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania, leo tarehe 26 Februari, 2021 katika uzinduzi wa ushirikiano wa programu ya mafunzo kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Chama cha Skauti Tanzania Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji Dodoma. (Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
DODOMA,
Imeelezwa kuwa kati ya Mwezi Julai na Disemba mwaka 2020 kulikuwa na matuko ya moto 35 kwenye shule mbalimbali na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na vifo vya wanafunzi 13.
Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika matukio hayo ulibaini kuwa vyanzo vya matukio ni matumizi ya umeme kwa njia zisizofaa, migogoro ya wanafunzi na walimu, jamii zinazowazunguka zinazopelekea hujuma, uchakavu wa miundombinu ya umeme, kutokuwa na mifumo ya kinga na tahadhari ya moto kwenye majengo, baadhi ya matukio kutogundulika vyanzo vyake pamoja na baadhi ya shule kutokuwa na walinzi jambo ambalo ni hatari kwa usalama.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo John Masunga wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa programu ya mafunzo kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Chama cha Skauti Tanzania ambapo amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa majanga ya moto yanadhibitiwa wataendelea kutoa elimu na kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto.
Naye Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Khamis Hamza Chilo (Mb) amesema Wizara hiyo imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za makusudi kusimamia na kuhakikisha majanga hayo yanadhibitiwa ili kulinda maisha ya watu pamoja na mali zao.
Kwa upande wa Skauti Mkuu wa Tanzania Mwantumu Mahiza amesema kutokana na shule nyingi kukumbwa na majanga ya moto mara kwa mara imepelekea wao kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa elimu kwa vijana ili kuepusha uharibifu wa rasimali zote.
Akizindua leo Ushirikiano wa Programu ya Mafunzo kati ya Jeshi hilo na Chama cha Skauti, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe Seleman Jafo (Mb) amesema hivi karibuni kumeshuhudiwa uharibifu mkubwa wa miundombinu kutokana na majanga ya moto hasa katika Majengo ya serikali pamoja na shule mbalimbali hapa nchini hivyo kwa ushirikiano walioufanya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na chama cha Skauti itasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na majanga hayo .
Toa Maoni Yako:
0 comments: