Mtumishi wa Mungu Mwalimu Joyce Mwakalasya baada ya kutoa mafunzo ya upandaji wa mbegu kwa waumini wa Kanisa la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam Jumapili.
Mchungaji wa Kanisa la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam, Raphael Mwampagatwa (kulia) akiwa na Mtumishi wa Mungu Mwalimu Joyce Mwakalasya (katikati) baada ya kutoa mafunzo ya upandaji wa mbegu. Kushoto ni mke wa mchungaji huyo.
Waumini wa kanisa hilo wakifurahi.
Waumini wa kanisa hilo wakibadilishana mawazo baada ya mafunzo hayo. Katikati ni mmoja wa Wazee wa kanisa hilo, Mwalimu Mary Anyitike.
Na Dotto Mwaibale
WAKRISTO wametakiwa kupanda mbegu bora kwa kumtolea Mungu sadaka ili waje wavune mavuno mengi.
Ombi hilo limetolewa na Mtumishi wa Mungu Mwalimu Joyce Mwakalasya wakati akitoa mafunzo ya upandaji wa mbegu kwa waumini wa kanisa la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam Jumapili.
Mwakalasya alisema suala la upandaji wa mbegu ni la muhimu wakati wa kumtolea Mungu sadaka kwani huwezi ukatoa sadaka ndogo wakati unayo kubwa ukategemea kubarikiwa.
"Hata kabla ya kwenda kutoa sadaka yako Mungu anakuwa anaijua hivyo tunapokwenda kuitoa mbele ya madhabahu tutoe kwa uaminifu ili uje uvune mavuno mengi baada ya kuipanda." alisema Mwakalasya.
Alisema kabla ya kupanda mbegu yako hiyo unapaswa kujua unaipanda eneo gani na kwa wakati upi na si kila eneo utakapo ipanda itastawi.
Mwakalasya alitaja uvivu na uzembe kwa mkristo kuwa ni adui mkubwa wa upandaji mbegu hivyo alitoa rai ya kufanya kazi kwa bidii kwani huwezi kumtolea Mungu sadaka bila ya kuwa cha chanzo cha mapato.
Alitaja vitu vingine ambavyo vinakwamisha kupanda mbegu ni mtu kuwa na imani haba, wivu usiofaa, uchoyo, ubinafsi, kutosamehe, kufanya kazi isiyo halali na kutolipa kodi ya serikali.
Alitaja changamoto nyingine zinazo changia kuzolotesha upandaji wa mbegu kuwa ubinafsi, hofu, kutokuwa na moyo wa kuthubutu kufanya jambo, kiburi, ushirikina na kuwaza kinyume cha matokeo.
Alisema mkristo akifanikiwa kuyashinda mambo hayo ni lazima atapata mafanikio Mungu ni zaidi ya yote kwani aliweza kuwa saidia akina Eliya na wengine wengi hivyo ukimtolea sadaka kamilifu kwa kupanda mbegu atakubariki.
Mwakalasya alitumia nafasi hiyo kuwaambia waumini hao kuwa mara baada ya kuvuna mavuno yao yaliyotokana na upandaji mbegu wayatumie kuwa saidia watu wenye uhitaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments: