Naibu Waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundi akisisitiza jambo wakati wa ziara yake kwenye Kijiji cha Msaraza wilayani Pangani kulia ni Meneja wa Wakala wa maji Safi na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA wilayani Pangani Zuberi Yahaya katikati aliyevaa suti ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange wa kwanza kulia aliyevaa kofia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundi katikati akikata utepe kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji Mbulizaga kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange na wa kwanza kuli ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundi katikati akiingia kwenye feri wilayani Pangani wakati wa ziara yake wilayani humo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundi akizundua mradi wa Maji wa Kijiji cha Mbulizaga wilayani Pangani wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kushoto ni Meneja wa Wakala wa maji Safi na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA wilayani Pangani Zuberi Yahaya Naibu Waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundii
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundi kulia akimsikiliza Meneja wa Ruwasa wilaya ya Pangani Zuberi Yahaya na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundi kulia akimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundi katikati akiteta jambo na katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange wakati wakivuka kivuko cha MV Pangani katika ziara yake ya siku moja wilayani humo kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundi amemtaka Meneja wa Wakala wa maji Safi na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA wilayani Pangani Zuberi Yahaya kujitathimini utendajikazi wake kutokana miradi ya maji kushindwa kutekeleza kulingana na kasi inayotakiwa. 

Agizo hilo alilitoa baada ya kukagua miradi ya maji ya katika kijiji Cha Msaraza na Mkalamo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji wilayani Pangani

Alimtaka Meneja huyo kujitathimini kama nafasi hiyo anaiweza kwani miradi imeshindwa kutekelezwa huku wananchi wakiendelea kuteseka na kero ya ukosefu wa maji Safi na salama. 

"Tunapaswa kukuondoa sio ndio lakini niwaambie wataalamu acheni kufanya kazi kwa mazoea nyie wataalamu siasa katika ufanyajikazi sio nzuri kwani wananchi wanahitaji maji sio maneno tuuu" alisema Waziri huyo.

Aliwataka watendaji wa Ruwasa kuachana na kufanyakazi kimazoea bali wafanyakazi kwa kasi ambayo itaharakisha maendeleo na wananchi kupata huduma ya maji Safi na salama.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja RUWASA wilaya ya Pangani Rajab Yahaya alisema kuwa wakala huo unatekeleza miradi mitano ya maji katika wilaya hiyo ambalo utakapokamilika utasaidia kuongeza kiwango cha huduma kutoka asilimia 35%hadi 80%.

Hata hivyo aligusia suala la kusuasua kwa miradi ya Msaraza na Mkalamo ambapo alisema imechelewa kutokana na ucheleweshaji wa fedha za miradi hatua ambayo imeshindwa kuendelea kama ilivyopangwa.

Alisema kuwa Licha ya kuwepo kwa vifaa lakini fedha za kuwalipa mafundi zilichelewa hali ambayo imesababisha miradi hiyo kusimama kwani wanapofanya kazi wanapaswa kulipa siku hiyo hiyo.

Hata hivyo kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa maji Safi na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA mkoani Tanga Mhandisi Upendo Lugongo alisema kuwa tayari wamelichukua hilo na kuhaidi kulisimamia kuanzia Jumanne mradi utekelezwe ili uweze kukamilika ifikapo mwezi Machi 2021 mwaka huu ili wananchi waweze kupata maji.

Mhandisi Upendo alisema awamu ya pili wameshafanya usanifu Mkalamo na umefika mwisho hivyo watu wa Mkalamo baada ya awamu ya kwanza kwisha awamu ya pili itakayoanza mwaka 2021/2022 nao wapo kwenye mpango watapatiwa maji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: