Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association (TAHA) iliyofanyika katika mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.

Meneja miradi Taasisi ya Tanzania Horticultural Association (TAHA) Bi. Elianchea Shanga akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa taasisi ya TAHA iliyofanyika katika mjini humo.

Wakulima wa Mboga Mboga akinyoosha mikono kujitambulisha.

 Meneja mradi Naimana akizungumza wakati akitambulisha mradi huo huku wakulima na wageni waalikwa wakifuatilia.
 Mmiliki wa shamba la nyanya la kisasa akiongea machache.
Meneja miradi TAHA Bi. Elianchea Shanga akiwatambulisha mabwana shamba wanaosaidia kufundisha wakulima.
 Wafanyakazi wa TAHA wakitoa elimu kwa wakulima.
 Kilima cha kisasa cha nyanya.
 Mgeni rasmi Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akipewa maelezo juu ya kilimo cha kisasa cha nyanya kutoka kwa Meneja mradi huo Naimana.
 Vingozi wa kijiji wakiwa na Mgeni rasmi.
Wakulima wakiwa na mgeni rasmi.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.

Watafiti wa mazao ya kilimo nchini wametakiwa kuhakikisha tafiti zao zinawafikia wakulima wadogo wadogo hasa waliopo vijiji ili wakulima hao waweze kulima kilimo chenye tija ikiwa ni katika kubabiliana na changamoto ya ushindani wa masoko kitaifa na kimataifa.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba, wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association (TAHA) iliyofanyika katika mjini Morogoro.

Bi. Chumba amesema kuwa watafiti hao endapo watafanya zao vyema zinaweza kumkomboa mkulima na akaweza kupata soko bora la mazao yao na itawakwambua kiuchumi.

"Niwashukuru wataalamu maana nyie mmekuja wakomboa wakulima wadogo ambao mara nyingi huwa ni  ngumu kufikiwa matokeo yake wamekuwa wakilima kilima cha mazoea ambacho hakina manufaa kwao," amesema.

Nae Meneja Miradi ya Taasisi ya TAHA, Bi. Elianchea Shanga amesema kuwa kwa sasa wamesambaa mikoa mbali mbali ya Tanzania na lengo lao kubwa ni kumkomboa mkulima kutoka katika kilimo cha mazoea na kulima kilimo cha tija.

"Sisi lengo kubwa mkulima aone dhamani ya kile anachokilima maana tunasimamia kuanzia kuandaa shamba, madawa na mbolea huku tukimpa ushauri na kumtafutia soko," amesema.

Kwa upande wao wakulima Mwajuma Abdala wamefurahishwa na ujio wa Taasisi ya TAHA huku wakielezea kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa mwiba kwao kwa sasa ni mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yamepelekea ukosefu wa mvua huku wakiiomba serikali kuongezea nguvu katika kusaidia kilimo cha umwagiliaji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: