Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mh Edward Mpogolo leo Ofisini kwake,mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli kufuatia .Mh Edward alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma. 
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mh Edward Mpogolo vitendea kazi leo Ofisini kwake,mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli.Mh Edward alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma. 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mh Edward Mpogolo akitia saini kiapo chake mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singinda Mh Dkt.Rehema Nchimbi.

MKUU mpya wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Bw Edward Mpogolo ameapishwa leo rasmi kuanza majukumu yake kama Mkuu wa Wilaya hiyo, kuchukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Miraji Mtaturu ambaye kwa sasa ni Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu jana, uteuzi wa Bwana Mpogolo ulianza rasmi jana Julai 24, 2019, kuwa mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.

Baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi Rehema Nchimbi, Mpogolo ameahidi kushirikiana na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya katika kuhakikisha inakuwa na maendeleo sambamba na kusimamia kikamilifu makusanyo ili kuinua uchumi wa eneo hilo.

“Ninamskuru Rais Dk,John Magufuli kwa kuniteua,ninaahidi kuwa sitamwangusha ,nitahakikisha ninashirikiana na Uongozi wa Mkoa na Halmashauri yangu ya Ikungi ili kuhakikisha tunafikia malengo ya makusanyo katia Wilaya yetu”amesema Mpogolo.

Ameahidi kushirikiana na uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ili kuhakikisha wanatumikia wananchi wa Wilaya hiyo ikiwa wao ndio wawakilishi wa Rais katika eneo hilo.

Pia ameahidi kwenda kuisimamia Katiba ya Nchi pamoja na Ilani ya Chama Tawala, Chama Cha Mapinduzi katika kuwatumikia wananchi atakaowaongoza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amesema Mkuu wa Wilaya ndio msimamizi mkuu wa Kamati ya ulinzi na usalama na ndio msimamizi mkuu wa shughuli za maendeleo katika eneo husika na kumtaka kwenda kusimamia vyema miradi ya Serikali inayotekelezwa Wilayani humo.

“Mkuu wa Wilaya yeye ni msimamizi mkuu na muwakilishi wa Rais katika Wilaya na ndio mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama na ukasimamie miradi yote inayotekelezwa Wilayani humo” amesema Dtk Rehema..
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: