Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa kazi (OSHA) Paul Gyuna (kushoto) akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga wakati alipotembelea banda laob kunakoendelea kuna kofanyika maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifankwenye viwanja vya Tangamano mjini hapa
Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao.
Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao.
Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akimpima urefu mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao.
Kutokuzingatiwa kwa usalama na afya sehemu za kazi kunaweza kuleta athari kubwa ya kiuchumi kwa wafanyakazi kutokana na kwamba wanaweza kukumbana na majanga makubwa hali inayopelekea kuathiri shughuli zao na kila siku na kujirudisha nyuma kimaendeleo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa kazi (OSHA) Paul Gyuna wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga kunakofanyika maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa.
Amesema wanatumia maonyesho hayo ya wiki ya vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo wamedhamiria kuwaeleza fursa wanazoweza kuzitumia ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Tunaangalia Usalama na Afya kwenye maeneo yao ya kazi…tunaelewa wameajiriwa lakini kuna changamoto nyingi wanazopita kutokana na kwamba wengi hawaelewi kuhusiana na mambo ya usalama na afya na kutokujua jinsi ya kujikinga na madhara hivyo tumekuja kutoa elimu”Alisema.
Amesema elimu wanayoitoa kwenye maonyesho hayo wanaamini wananchi wakishaijua wanaweza kujiepusha na athari za kazi hata ufanisi wa kazi utaongezeka na kuongeza kipato hatua itakayosaidia kuinua uchumi wao na jamii zinazowazunguka.
Hata hivyo alisema pia licha ya kutoa elimu hiyo lakini wanatumia wiki hiyo kufanya upimaji wa afya, presha uzito na urefu na kutoa ushauri ili kuweza kuwasaidia kuondokana na matatizo wanayokutwa nayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: