Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa {Katikati} akiongea na waandishi wa Habari (hawapo Pichani) kuhusiana na fursa mbalimbali za biashara zinatazopatika katika mkoa huo kutokana na ujio wa tamasha la Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ya wiki katika viwanja vya Nangwanda Sijaona. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa na Mratibu wa Tamasha la Tigo Fiesta, Pancras Mayalla almaarufu Askofu TZA.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa {Kulia}akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa {katikati}pamoja na Mratibu wa Tigo Fiesta 2918 , Pancras Mayalla almaarufu Askofu TZA katika Mkutano na waandishi wa habari kueleza maandalizi ya tamasha la Tigo Fiesta 2018 litakalofanyika uwanja wa Nang'wanda Jumapili hii pamoja na ofa mbali mbali za kampuni ya Tigo katika msimu huu ikiwemo mfumo wa malipo kwa wakulima wa korosho kupitia huduma za Tigo Pesa.
---
Huku msimu wa mavuno ya korosho ukiwa umewadia katika mikoa ya nyanda za juu kusini, wakaazi wa Mtwara na viunga vyake wanajiandaa kuvuna vibe kama lote kutoka kwa mastaa wa muziki wa bongo flava katika msimu unaoendelea wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote.

Waandaaji Clouds Media Group, kupitia Katibu Kiongozi wa Kamati ya Maandalizi, Gardner Habash amewaalika wakaazi wa Mtwara waje kupumzika baada ya shughuli ngumu za kuvuna korosho kwa kusikiliza 100% vibe za nyumbani. 

‘Kwa wafanya biashara, msimu waTigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ni fursa ya kujiongezea kipato kwa kutoa huduma za usafiri, malazi, vinywaji na chakula na huduma nyingenezo zinazohitajika na maelefu ya mashabiki watakaojitokeza kushuhudia tamasha hili,’ Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byanakwa alisema. 

Kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota, wasanii wanaochipuka kutoka Mtwara watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao, na wale watakaofanya vizuri watapewa fursa ya kutumbuiza katika tamasha kuu la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote linalotarajiwa kurindima siku ya Jumapili tarehe 14 Oktoba katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. 


Watakaoshusha vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki mjini Iringa. Wengine ni wasanii a bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva. 


TIketi za Tigo Fiesta 2018 – Mtwara zinapatikana kwa bei punguzo ya TSH 5,000 kupitia Tigo Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika cha TSH 5,000 kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888. 

Tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote tayari limezuru mikoa ya Morogoro, Sumbawanga na Iringa, na linatarajiwa kutembelea mikoa ya Singida, Songea, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku fainali ikiwa Dar es Salaam. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: