Waziri Wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akikagua vipando vya Pamba mara baada ya kutembelea maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi katika viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza, Leo tarehe 7 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
Waziri Wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza kupunguzwa gharama za mbegu alipotembelea banda la kampuni ya Risk Ziwaan kwenye maonesho ya kilimo na sherehe za Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi katika viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza, Leo tarehe 7 Agosti 2018.
Waziri Wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea banda la Bodi ya Pamba kwenye maonesho ya kilimo na sherehe za Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi katika viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza, Leo tarehe 7 Agosti 2018.
Na Mathias Canal, WK-Mwanza.
Waziri Wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba leo Agosti 07, 2018 ametembelea maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika katika uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza.
WAaziri Tizeba amewataka washiriki wanaoonesha bidhaa mbalimbali za kilimo kuwa wakweli kwa wakulima ili kutoka elimu kwani wamekuwa wakitoa maelezo mbalimbali juu ya bidhaa zao wakiwa katika mtazamo wa kibiashara zaidi pasina kutoka elimu na mafunzo kwa wakulima.
Akizungumza na baadhi ya wananchi waliomlaki katika viwanja hivyo Waziri huyo anayeshughulikia sekta ya kilimo amesema kuwa gharama za bidhaa mbalimbali katika maonesho hayo ziko juu hivyo wakulima wanapaswa kupunguza gharama za bidhaa hizo.
Akiwa katika banda la kampuni ya Risk Ziwaan ameitaka kampuni hiyo kupunguza gharama za mbegu za mbogamboga na matunda ili kuwa na gharama rafiki kwa wakulima ili kuongeza tija katika uzalishaji na ukuzaji wa sekta ya kilimo nchini.
Alisema kuwa serikali imefuta kodi na tozo mbalimbali kwenye sekta ya kilimo lakini bidhaa za kilimo bado zinauzwa kwa gharama kubwa jambo ambalo ni kinyume kabisa na matarajio ya serikali.
"Kama tumefuta Kodi na tozo ni kwanini wafanyabiashara wa mbegu bado wanatunisha misuli pasina kupunguza bei, endapo wakiendelea hivyo pasina kupunguza bei tunapoelekea tutafuta leseni zao za biashara au kurejesha tozo na Kodi" Alikaririwa Mhe Tizeba.
Hii ni mara ya kwanza maonesho ya Kanda ya Ziwa Magharibi yanayoshirikisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera kufanyika baada ya serikali kugawa mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kanda mbili kwa ajili ya kushiriki maonesho ya Nane Nane. Kanda nyingine ni Kanda ya Ziwa Mashariki inayoshirikisha mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.
Kilele cha Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu ambapo Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Benjamin Willium Mkapa ndiye Mgeni rasmi katika killele chake.
Toa Maoni Yako:
0 comments: