Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Exaud Mamuya (katikati) akiwakatika vazi maalumu baada ya kuchaguliwa kwamara nyingine kushika nafasi hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini.
DIWANI wa kata Marangu Mashariki katika jimbo la Vunjo,Mh Exaud Mamuya amechaguliwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi baada ya kushinda kwa kura 45 zilizopigwa .
Katika kinyang’anyiro hicho, Mh Mamuya alikuwa akichuana na wagombea,Filbert Shayo kutoka chama cha NCCR-Mageuzi na Chata Madata wa Chama cha Mapinduzi ambaye hata hivyo baadae alienguliwa.
Akizungumza wakati wa Uchaguzi huo, Afsa Uchaguzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Patrick Nyavanga alitoa ufafanuzi wa namna mshindi anavypatikana katika uchaguzi huo ikiwemo mshindi kupata kura za ndio zisizopungua asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa.
Alisema uchaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa kifungu namba 6 cha kanuni za kudumu za Halmashauri na baraza la madiwani wa Halmashauri wa Wilaya ya Moshi likaridhia kufanyika kwa uchaguzi wa Makamu mwenyekiti.
Uchaguzi huo ulilazimika kufanyika kwa awamu mbili baada ya awamu ya kwanza kukosekana mshindi baada ya wagombea wote kutofikisha zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa.
Katika marejeo ya awamu ya piliya zoezi la upigaji kura jumla yakura 45 zilipigwa ambapo Mh, Mamuya alipata kura 45 baada ya mgombea kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi Mhe, Shayo kuamua kujitoa wakati wa uchaguzi wa marudio na Mhe.Chata kuenguliwa.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi Peter Malendecha alimtangaza Mhe.Exaud Willison Mamuya mgombea kwa tiketi ya CHADEMA kuwa Makamu Mwenyekitiwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwakipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.
Akizuzngumza mara baada ya kumtangaza mshindi,Malendecha alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki na umeendeshwa kwa amani na utulivu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uchaguzi.
Mbali na uchaguzi huo baraza la madiwa wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi limeunda kamati na kufanya uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbalimbali za kudumu za Halmashauri ikiwemo kamati ya Elimu ,afya na maji, kamati ya maadili, kamati ya mipango miji na kamati ya Uchumi, ujenzi na mazingira.
Toa Maoni Yako:
0 comments: