Na Agnes Francis, blogu ya Jamii.
Kamati ya waamuzi ya shirikisho la soka la Tanzania (TFF) limewasimamisha badhi ya waamuzi ambao wamefanya makosa kwenye michezo ya raundi ya kwanza na ya pili ligi kuu Tanzania Bara (TPL).
Kupitia kwa Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) Salum Chama amesema wasimamizi hao wamesimamishwa kupisha uchunguzi kwa kosa la kukataa magoli ya mechi zilizochezwa hivi karibuni.
Muamuzi msaidizi line 2 Godfrey Msalala kutoka Geita alikataa goli la Makambo katika mchezo dhidi ya Yanga na Mtibwa sugar kwa kudai kuwa mfungaji alikuwa ameotea,Sylvester Mwanga kutoka Kilimanjaro line 1 amesimamishwa pia kwa kosa la kulalamikiwa kuzuia shambulizi la Mtibwa akidai Ismail Aidan alikuwa ameotea huku picha za video za marudio zikionyesha hakuotea.
Muamuzi a Kati Nassoro Mwinchui na msaidizi wake Abdallah Rashidi wa Pwani wamekata goli la Biashara United gemu waliocheza na Coastal union ambapo walidai kuwa mchezaji alikuwa amekwishakuwa katika eneo la kuotea goli.
Vile vile pia muamuzi msaidizi Nicholas Makanya wa Morogoro alikataa bao la ruvu shooting dhidi ya KMC akidai mfungaji Fully Zungu alikuwa kwenye nafasi ya kuotea.
Salum Chama amesema waamuzi hao walichezesha Mpira chini ya kiwango na kupata Alana chache zilizopelekea kusimamishwa kupisha uchunguzi Kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.
Hata hivyo kamati ya uendeshaji wa ligi ya Tanzania bara (kamati ya saa 72) itakaa na kufanya uchunguzi na itatangaza hatua wakazochukua,iwapo itabainika waamuzi hao wamefanya makosa katika mechi hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: