NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi kombe la Ubingwa wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup nahodha wa timu ya TOC Bato Diasi kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama aliyevaa koti jeupe.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto akimvalisha medali mchezaji wa timu ya Ushirika FC ambao walishika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Kombe la Aweso Cup kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akimkabidhi sh.50000 Twaha Bungala ambaye ni mfungaji bora kwenye mashindano hayo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso katikati akimkabidhi kitita cha sh.milioni 1 nahodha wa timu ya TOC Bato Diasi juzi ambao niMabingwa wa Ligi ya wilaya hiyo maarufu kama Aweso Cup iliyodhaminiwa na Mbunge huyo.
Na Mwandishi Wetu.
TIMU ya TOC FC juzi walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup baada ya kuifunga Ushirika FC mabao 4-3 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye viwanja vya Kumba wilayani Pangani.
TOC ambao ni mabingwa walikabidhiwa kombe la Ubingwa,Medali na kitita cha sh.milioni 1 kutoka kwa mdhamini wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo (CCM).
Huku mshindi wa pili timu ya Ushirika FC walikabidhiwa kitita cha laki sita na medali wakati mshindi wa tatu akipata laki nne na medali kwenye tukio ambalo lilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.
Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kushindwa kutambiana ndani ya dakika tisini na hivyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ndipo TOC walipofanikiwa kuibuka videdea.
Toa Maoni Yako:
0 comments: