Semina ya Mawakala wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2011 itafanyika tarehe 29 na 30 April 2011 katika hotel ya Paradise City iliyopo Posta jijini Dar es salaam.


Semina hii itahusisha Mawakala wote wa Mikoa, na Kanda wanaoandaa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.

Katika semina hiyo ambayo pia itakuwa ni Mkutano wa mwaka wa Waandaaji wa Miss Tanzania katika ngazi za Mikoa na Kanda, mambo kadhaa yatazungumzwa ikiwemo, kukumbushana Kanuni, Sheria na Taratibu za Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, maadili na miiko ya uongozi, na uendeshaji wa mashindano.


Pia Changamoto mbalimbali zinazokabili mashindano ya urembo zitajadiliwa. Mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu kutoka katika Fani ya urembo na Taasisi mbalimbali.

IMETOLEWA NA;


HASHIM LUNDENGA.

MKURUGENZI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: