Mkurugenzi wa Kampuni ya Ceragem, Africa Mashariki, Nam Chae Woo,(kulia) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Dafa Ceragem, Edmund Mndolwa jinsi  mashine mpya ya Ceragem V3 inavyofanya kazi , wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo inayotumia teknolojia ya hali ya juu katika kutibu magonjwa mbalimbali bila ya mgonjwa kumeza dawa au kuchomwa sindano katika vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini . Anaeshuhudia ni Patricia Mndolwa.
 Mzee Fransis Kavishe na Bi Ashura Salum,wanaosumbuliwa na ugonjwa wa
kansa wakifunua kitambaa, kuashiria uzinduzi wa Mashine mpya ya Ceragem V3  inayotumia teknolojia ya hali ya juu katika kutibu magonjwa
mbalimbali bila ya mgonjwa kumeza dawa au kuchomwa sindano katika vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini,pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Dafa Ceragem, Edmund Mndolwa, Mkurugenzi wa Kampuni ya Ceragem, Africa Mashariki, Nam Chae Woo, na Patricia Mndolwa.
 Mzee Fransis Kavishe na Bi Ashura Salum,wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kansa wakikata utepe, kuashiria uzinduzi wa Mashine mpya ya eragem V3 inayotumia teknolojia ya hali ya juu katika kutibu magonjwa mbalimbali bila kumeza dawa wala kuchomwa sindano katika vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini,Pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ceragem, Africa Mashariki, Nam Chae Woo, Mkurugenzi wa Dafa Ceragem, Edmund Mndolwa.
 Baadhi ya Wagonjwa na wafanyakazi wa Kampuni ya Ceragem, Africa
Mashariki wakifuatilia hotuba ya Uzinduzi waMashine mpya ya Ceragem V3  inayotumia teknolojia ya hali ya juu katika kutibu magonjwa mbalimbali bila ya mgonjwa kumeza dawa au kuchomwa sindano katika vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Ceragem, Africa Mashariki, Nam Chae Woo,  akizungumza na baadhi ya wagonjwa na wafanyakazi wa Dafa Ceragem wakati
wa Uzinduzi wa Ceragem V3 inayotumia Teknoloji ya hali ya juu katika
kutibu Magonjwa mbalimbali bila kumeza dawa wala kuchomwa sindano katika
vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini.Katika
picha kutoka kushoto, Patricia Mndolwa,  Mkurugenzi wa Dafa Ceragem,
Edmund Mndolwa, na Mgeni Mualikwa Bi. Lydia Mushumbusi.
 Wananchi waliofika eneo la tukio wakijaribu kuweka kumbukumbu....
 Moja ya mguu ulikokuwa kwenye mfuko huo.
Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanane kuhusiana na tukio la kuokotwa viungo vya binadamu katika eneo la Bunju A jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa watu wanane wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Kova amesema kuwa jopo la Wataalamu saba limeundwa kuchunguza tukio hilo na amethibitisha kuwa viungo vile vilikuwa ni vya maiti,ambavyo hutumika na madaktari kwa elimu ya matibabu na utafiti.

DSC_0248
Habari Marafiki, Wapenzi na Mashabiki nimeingizwa kwenye mashindano ya nani mkali Clouds Tv ni mwanamke pekee kwenye kinyang’anyiro kumtafuta Mwanamuziki bora wa bendi wa mwaka.

Tafadhali sana nahitaji sana kura zenu ili niweze kushinda.
Kupiga kura tuma sms andika MKALI 1 kisha tum kwenda 15678 hapo utakua umenisapoti sana mtu wangu wanguvu, love you all.

Mary Lucos wa Skylight Band.
Na Mwandishi Wetu.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka katika chama chake hawatashiriki katika Bunge hilo linalotarajiwa kuendelea mwezi ujao.

Aidha, amesema Chadema haitashiriki katika kikao cha Julai 24 kilichoitishwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta akisema hicho ni sehemu ya Bunge hilo ambalo wajumbe wake na wenzao wanaounda Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa) walilisusia.

Akisoma tamko la Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbowe alisema iwapo Bunge hilo litapitisha Rasimu ya Katiba Mpya isiyotokana na maoni ya wananchi, chama hicho kikiwa sehemu ya Ukawa, kitafanya kampeni nchi nzima kuwashawishi wananchi kuikataa wakati wa upigaji wa kura ya maoni.

Alisema kuliko kupata Katiba Mpya ambayo ni mbovu ni bora mchakato wa kuipata uchelewe ili Ukawa waendelee kupigania Katiba bora itakayopatikana kutokana na maoni ya wananchi na siyo maoni ya CCM.
Ilikuwa mnamo Julai 20, 2014 mara baada ya kumaliza sherehe za harusi katika ukumbi wa JKT MGULANI jijini Dar es Salaam nikatembea kwa mguu hadi kituo cha daladala, nilipofika kituoni ikapita haice na waliponiona konda akasema unaenda wapi nikamjibu Kariakoo, basi nikafunguliwa mlango na kuingia na kukaa kwenye siti na kulikuwa kuna abiria saba.

Mara baada ya kuwa nimekaa nikasikia sauti nikiambiwa oya tupo kazini hapa toa vyetu, mimi nikajua nauli nikatoa shilingi mia tano ili nilipe, mara nikatolewa panga na mwingine akatoa bastola na kusema nitoe fedha zote nilizonazo na niwape simu, kiukweli nilikuwa sina jinsi kabisa kwani nilikuwa kwenye kumi na nane zao.

Nikawapa simu na vijihela nilivyo navyo na wakanisachi ili kuhakikisha kuwa hawaniachi hata na senti moja, waliporidhika wakasimamisha gari, ila mmoja akasema si tumpe hata alama kidogo, basi wakati huo nilimwomba Mungu na kwa bahati nzuri wakanishusha na wakaondoka zao, kwa kuwa sikuwa na fedha tena basi nikatembea tu kurudi nyumbani.

Pole sana Deo Julius kwa tukio hili lililokukuta.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula (kushoto) akisaidiana na Meneja wa Kampuni ya utengenezaji wa vinywaji baridi vya Pepsi Mwanza, Nicolas Coertz  wakikagua utaratibu wa zawadi pamoja na vitendea kazi vya michuano ya Pepsi kombe la meya 2014 kabla ya kuvikabidhi kwa viongozi wa timu 22 zitakazo shiriki michuano hiyo.
Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, G. Sengo akitoa utaratibu utakao fuatwa kabla ya makabidhiano.
Mstahiki Meya aliiongoza meza kuu.
Mfungaji bora wa mashindano kuondoka na kitita cha shilingi laki mbili.

Timu yenye nidhamu itaondoka na kitita cha shilingi laki mbili.
Zawadi ya refa bora wa mashindano shilingi laki mbili, ile hali mshindi wa tatu atalitwaa kombe, medali ya shaba na kitita cha shilingi milioni moja.

Ni makombe na medali zake kwa michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014.
Uchapishaji kwa zawadi ya mshindi wa kwanza (kushoto) ulikosewa ni shilingi milioni moja na nusu (1500,000/=) ndizo atakazo ondoka nazo bingwa wa Pepsi Kombe la Meya 2014 ambapo mbali na kitita hicho pia bingwa huyo atakabidhiwa Kombe, medali ya dhahabu na bajaji ya kisasa ya mizigo yenye uwezo wa kubeba pia watu wanne yenye thamani ya shilingi milioni 4.5, huku mshindi wa pili wa michuano hiyo akiondoka na kombe, medali ya fedha na kitita cha shilingi milioni mbili.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akipakua chakula wakati  futari iliyoandaliwa na ofisi yake katika hoteli ya serena leo
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na Mfuko huo wa Pensheni wa PPF leo.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akitoa hotuba kwa wafanyakazi wa Mfuko huo baada ya futari iliyoandaliwa na Ofisi yake kwa wafanyakazi wake kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Pembeni ni Msimamizi wa Masoko wa mfuko huo wa Pensheni wa PPF, Bw Alfred Elia

 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakishiriki futari iliyoandaliwa na Mfuko huo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI (ASSISTANT INSPECTOR OF IMMIGRATION).

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, anawatangazia wafuatao waliofaulu usaili wa kujaza nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji (Assistant Inspector of Immigration) wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Mtaa wa Loliondo Kurasini, Dar es Salaam tarehe 29 Julai 2014, saa 2:00 asubuhi. Aidha, wahusika wote wanaelekezwa kufika kwa wakati wakiwa na vyeti halisi vya masomo na vya kuzaliwa.

1 Abel Md. Maganya
2.Absolum Stafford Bashigwa
3 Agnes P. Mlay
4 Ali Musa Abdallah
5 Angela Kagaruki
6 Antony J. Nyagilo
7 Asteria Kiyanga
8 Awadhi Issa
9 Aziza Kaku
10 Bakari M. Khamis
11 Baraka Estomihi
12 Beatrice K. John
13 Bernard K. Mwampashe
14 Binasra J. Sabri
15 Charles M. Swai
16 Cosmas J. Mbuguni
17 Dativa J. Ndyetabura
18 David Muna
19 Doroth Ngai
20 Dotto Tabu
21 Emmanuel Gelison
22 Ezekiel A. Kibona
23 Fahamu Saidi
24 Farida Sued
25 Felix Mkemwa
26 Forget N. Charles
27 Frida N.Masomhe
28Gabriel M. Kamugisha
29 Gath E. Nyansambo
30 Gerald Moses
31 Gideon Kihoko
32 Godson Mwanawima
33 Grace C. Nyarata
34 Hamza Sanga
35 Hassan A. Mziray
36 Ibrahim Ally
37 Idd Mgoi
38 Joachim Joseph
39 John G. Mgayambasa
40 Joseph Gregory
41 Kennedy John
42 Khamis Moh'd Khamis
43 Kombo M. Ame
44 Kwame Charles
45 Lawi E. Kumburu
46 Mabrouk H. Thabit
47 Mangunda A. Kaporo
48 Marco Zacharia
49 Maria Agapith
50 Mateso Msigala
51 Meshack Mwaisela
52 Michael John
53 Miriam Mwakamele
54 Mlalama Fortinatus Amlima
55 Mussa Hemedi
56 Mwita Mwikwabe
57 Neema R. Mrope
58 Nyangoma Martin
59 Oscar Philip
60 Pasaka Wilson
61Pastory Packshard Mkongwa
62 Reagan H. Kawa
63 Rose Nseka
64 Senga Ally
65 Silvia Ngasoma
66 Sixtus Stephano Burashahu
67 Steven L. Kweka
68 Wendy Y. Mwalukasa
69 Witness Lwambo
70 Zulu P. Charles

Aidha, ni muhimu kufahamu kuwa uchaguzi wa walioitwa kwenye ajira umezingatia yafuatayo:

• Vipaumbele vya Idara ya Uhamiaji;
• Kutoa nafasi kwa waombaji kutoka Zanzibar;
• Ufaulu kuanzia alama 50 asilimia na kuendelea;
• Jinsia
Wasailiwa ambao majina yao hayamo kwenye orodha hii wafahamu kuwa hawakufanikiwa.

Atakayesoma tangazo hili amjulishe na mwenzake.
Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.

Zaidi ya dollar billion 121.6 kwa mwaka zimeweza kuokolewa nchini katika uingizaji wa mafuta baada ya kuanza kutumia mfumo wa uingizaji wa mafuta kwa pamoja ambao umeanza januari mwaka 2012.

Mfumo huo umeweza kuokoa muda wa kuweza kupakua mafuta bandarini kutoka siku 60 hadi tatu na pia udhibitiwa ubora wa mafuta umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Hayo amebainisha Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya udhibitiwa Nishati na maji (EWURA) Felix Ngamlagosi wakati akifungua mkutano wa wadau toka taasisi mbalimbali nchini na nje ya nchi kwa lengo la kujadili na kutoa maoni yao kuhusiana na mfumo huo ili kuweza kupunguza gharama katika uchumi na kwa mtumiaji.

Felix amesema kwamba mfumo huu una uhakika zaidi kwa kutoa takwimu sahihi katika mafuta yote yanayotumika kwa ajili ya matumizi nchini.

Naye mdau kutoka benki ya NMB bi Wende Mengele ameeleza kwamba kutokana na mfumo huu kutaweza kuleta faida kwa wananchi pamoja na kwa benki kutakuwa na mfumo mzuri unaoeleweka.

Hatahivyo EWURA bado wanaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa uchumi hadi ifikapo Agosti 4, 2014 mwaka huu na baada ya hapo kuanza kuyafanyia kazi kwa kuyaweka pamoja huku wakishirikiana na benki kuu.
Moja ya kichwa cha binadamu kilichotolewa kwenye mifuko hiyo.
Miguu iliyokaushwa ikiwa kwenye mifuko. Picha kwa hisani ya Daresalaam-yetu.blogspot 
Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika  mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
HABARI ZA AWALI TOKA KWA MASHUHUDA WA TUKIO:
Habari zilizotufikia usiku wa leo Julai 21, 2014 maeneo ya Bunju B jijini Dar es Salaam watu wawili ambao walikuwa na gari dogo aina ya Isuzu wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakiwa viungo vya binadamu ambayo walikuwa wamevifunga katika mifuko ya plastiki.

Mashuhuda waliokuwa eneo la tukio walisema waliona gari aina ya Isuzu ikiwa imesheheni viungo mbalimbali vya binadam ikiwemo miguu, mikono, vichwa n.k.Viungo hivyo vilikua ni vibichi na vinavuja damu na vilikuwa vinaenda kutupwa damp la Mpiji..

Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa dereva wa gari hilo alifanikiwa kumwaga viungo safari ya kwanza (Trip) eneo la shule ya Consolata ya Masista na aliporudi kumwaga awamu ya pili ndipo wananchi walipowaita polisi na kufanikiwa kumkamata dereva huyo.

Polisi wa Kituo cha Bunju A na Wazo waliamua kupiga risasi hewani ili kuweza kuwatawanya watu waliovamia Kituo cha Polisi Bunju A wakiwa na lengo la kumuua dereva aliyekamatwa akiendesha gari hilo lililokuwa limejaa viungo hivyo.

Endelea kufuatilia sakata hilo.
Na Mohammed Mhina, Handeni

Wataalamu wa kilimo wilayani Handeni katika mkoa wa Tanga, kesho watakutana kuweka mezani mapendekezo ya mazao mapya yatakayofaa kwa biashara kwa lengo la kuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja wilayani humo.

Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Muhingo Rweyemamu, amesema leo kuwa katika mkutano huo, wataalamu hao watapitia itifaki mbalimbali zilizofikiwa na kuanisha zao mbadala kwa biashara kati ya korosho na ufututa ama yote mawili badala ya kutegemea mahindi pekee kwa chakula na biashara.

Amesema kwa muda mrefu imebainika kuwa pamoja na kuwa zao la mahindi hulimwa sana wilayani humo, zao ambalo limekuwa halibadilishi hali ya uchumi kwa wakazi wa wilaya hiyo kwa vile zao hilo pia hutumika kwa chakula jambo ambalo amesema kama mwananchi ataamua kuuza kwa upande mwingine hukaribisha baa la njaa katika kaya yake.

Amesema kubatikana kwa zao mbadala kutawawezesha wananchi kuondokana na umasikini na wakati huo huo kuendelea kubaki na chakula cha kutosha hadi msimu mwingine wa kilimo tofauti na ilivyo sasa ambapo wananchi walio wengi huuza chakula chote ili kupata mahitaji mengine huku wakibaki bila chakula majumbani hadi kupelekea kuomba msaada serikalini.
Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.

Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wakusoma sayansi nchini Taasisi ya utafiti wa sayansi nchini wameanda ama onyesho yatafiti mbalimbali za kisayansi na kiteknolojia zizilizofanywa na wanafunzi wa shule za sekondari hapa nchini yenye lengo la kukuza uelewa kuhusiana na kusoma masomo ya sayansi.

Akizungumza na waandishi wa habari nchini Mkurugenzi wa Young scientists Tanzania Dkt Kamugisha Gozibert (Pichani) amesema kwamba wanafunzi hao wapatao 300 wataonyesha tafiti zao walizofanya kwa takribani miezi saba hadi nane.

Dkt Gozibert ameeleza kwamba maonyesho hayo yameambatana na zawadi mbalimbali ikiwemo na udhamini wa kusoma masomo ya elimu ya juukwa wale ambaotafitizitaonekanakuwakivutiakizuri.
Maonyesho hayo yanatarajia kufanyika Agosti 13 na 14 hapa jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
1970462_1454799778083088_1638018053_n
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendiya Vijana Jazz.
1486871_1427285270834539_2027172492_n
Marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vjana Jazz enzi hizo.
---
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana Vijana Jazz enzi hizo ambapo anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama ilikuwa kama kujifurahisha, Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo marehemu baba yake Mzee Hemedi Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.

Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake Hemed Maneti, Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana Hall Kinondoni.


Komweta mpaka sasa ana Nyimbo mbili na zipo mbioni kutoka akiwa ameimba kwa kushirikiana na bendi ya Vijana Jazz mtunzi akiwa ni yeye mwenyewe nyimbo yake Inaitwa (Walimwengu) na nyingine inaitwa (Nitajuaje) ukiwa ni utunzi wa Shomary Ally lakini yeye akiwa mwimbaji kiongozi katika wimbo huo pamoja naye Julius Mwesiwa.

Wanamuziki wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally, Abdallah Mgonahazeru na Roshy Mselela, Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad. 

Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama.

Ni kweli kwamba mara nyingi nakuwa nafanya kazi siku za wikiendi hivyo nakosa muda wa kutosha wa kukaa na mtoto ukizingatia ndiyo siku na yeye anakuwa anapumzika haendi shule, lakini kama mama unatakiwa kujua majukumu ya familia yako ninafurahia maisha na familia yangu na mtoto wangu ni mweye furaha sana ninamshukuru mungu kwa hilo,

hata hivyo siku za jumatatu zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika kumwandalia mahitaji yake kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa nimechoka na kazi.

Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa "Nashukuru Mungu sana kwa hilo na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu...watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza..."

Anamaliza kwa kusema "Umaarufu wa marehemu baba yake mzee Hemed Maneti upo na siwezi kuuepuka...lakini kubwa watu wananipima kutokana na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani".
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles
Singili akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya Azania,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA).


Bwa.Singili alisema kuwa Benki ya Azania ni kama sehemu ya jamii, watajitahidi kutoa msaada kwa jamii katika Nyanja za elimu,afya na kusaidia yatima kila nafasi na uwezo unaporuhusu.Benki ya Azania
pia iliwaalika Watoto waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House Foundation.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa  benki ya Azania imekuwa sasa na kufikia matawi 15 ikilinganishwa na matawi matatu waliyokuwa  nayo mwaka 2007,alisema kwa Dar es salaam pekee wana jumla ya matawi 05. ''tunawashukuru wateja wetu,kwani bila uwepo wao tuingefika hapa,tunapenda kuwahakikishia kuwa tunaendelea na juhudi zetu za nia ya kutaka kuwa na teknolojia ilio sahihi'',alisema MKurugenzi huyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Bw.Charles Singili (kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wageni wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo pamoja na waalikwa wengine kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar.
 Afisa mkuu maendeleo ya biashara kutoka benki ya Azania,Bwa.Othman Jibrea
akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar Es Salaam.
 Watoto waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House Foundation wakipata futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya Azania sambamba na wadau wengine wa benki hiyo,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar Es Salaam.
Sheikh Abdulrahman Ali Issa akitoa shukurani za dhati (kwa niaba ya sheikh wa Mkoa Dar Es Salaam),kwa uongozi wa benki ya Azania kwa kutoa mwaliko wa futari kwa wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo watoto yatima kutoka kituo cha Mitindo House Foundation..
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Bwa. Charles Singili (kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wageni wakipakua ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Mkali wa kuchekesha na sanaa za majukwaani Afrika Mashariki, Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kali hapo August 2, katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo linaloandaliwa na kituo cha Radio 5 litaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band, pamoja na mchekeshaji Fredi Omondi kutoka Kenya na Pilipili wa Tanzania.

Akizungumzia tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis alisema kuwa wameamua kumualika Kansiime kwa sababu ana kipaji cha hali ya juu katika uchekeshaji na ana mashabiki wengi Tanzania.

“Kansiime ni mchekeshaji ambaye amejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa uwezo wake wa kuweka utani kwenye maisha ya kawaida’ alisema Francis.

Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.

Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Burudani hii ya Kansiime, ambayo itakwenda kwa jina la Cheka Kwa Nguvu, itaanza saa moja usiku na tiketi zitauzwa shilingi elfu 90,000 kwa mtu mmoja, na shilingi 700,000 kwa meza ya watu nane.

‘Kama ambavyo mwandishi wa vitabu, Maya Angelou alivyowahi kusema, “Simwamini mtu yeyote asiye cheka” tukio hili linalenga kuonesha umuhimu wa kucheka katika maisha yetu ya kila siku” alihitimisha Francis.

Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Nasri Abu Jaish akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. 
Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Nasri Abu Jaish akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdul Sheriff akiwasilisha mada katika mkutano huo. 
Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdul Sheriff akiwasilisha mada katika mkutano huo.Sheikh Jalala (katikati) akizungumza katika mkutano huo. Sheikh Jalala (katikati) akizungumza katika mkutano huo.Meza kuu ikifuatilia majadiliano katika mkutano huo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. Meza kuu ikifuatilia majadiliano katika mkutano huo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina. Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina.Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina. Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina.


BALOZI wa Palestina nchini Tanzania, Nasri Abu Jaish amevitaka vyombo vya habari nchini Tanzania kusaidia kupaza sauti dhidi ya vitendo vya uonevu na mauaji yanayofanywa kwa raia wa Palestina na taifa la Israel ili vitendo hivyo vikomeshwe mara moja.

Balozi Abu Jaish ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliokutana na ubalozi huo kuzungumzia hali halisi ya mgogoro wa Palestina na taifa la Israel unaoendelea hadi sasa.

"...Mi naomba waandishi wa habari Tanzania andikeni ukweli juu ya uonevu huu wanaofanyiwa raia wasio na hatia, sitaki muandike kwa kupotosha semeni ukweli ili umma ujue nini kinachoendelea kwa Wapalestina ndani ya taifa lao...," alisema Balozi Abu Jaish akizungumza na wahariri hao.

Pamoja na hayo Balozi Abu Jaish aliiomba Tanzania na mataifa mengine yanayopenda amani kuungana kwa pamoja na kupaza sauti kukemea uonevu wanaofanyiwa raia wa Palestina ndani ya ardhi yao, kwani sauti za wengi zinaweza kukomesha hali hiyo na hatimaye mauaji kwa raia wasio na hatia kukoma mara moja.

Aidha alisema kitendo cha taasisi za kimataifa kukaa kimya huku raia wasiokuwa na hatia wakionewa na wengine kupoteza maisha ni sawa na kubariki vitendo hivyo viendelee. "...Makosa yanayofanywa na taifa la Israel yanaweza kuwa ya ulimwengu mzima endapo tutaendelea kukaa kimya huku watu wakionewa na kuuwawa nchini mwao...kama kweli hatupendi haya yaendelee kwanini tunakaa kimya," alihoji Balozi Abu Jaish.

Awali akiwasilisha mada kwa wahariri Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdul Sheriff alisema mgogoro wa Palestina na Israel unachochewa na ukandamizaji ulioanza kufanywa katika mgawanyo wa ardhi ya mataifa hayo tangu mwaka 1947.

Alisema chanzo cha Tatizo la Palestina lilianza tangu mgawanyo wa ardhi kati ya Wayahudi na Waarabu; katika mgawanyo huo waarabu ambao walikuwa wengi walipewa sehemu ndogo ya ardhi huku Wayahudi ambao walikuwa ni wachache walipewa sehemu kubwa ya ardhi.

Alisema mpango wa Mgao wa Palestina uliofanywa na Umoja wa Mataifa, UN mwaka 1947 uligawa nchi ya
Warabu milioni 1.2 walipewa ardhi kwa asilimia 43, huku idadi ya Wayahudi milioni 0.6 wakipewa ardhi asilimia 56 mgao ambao haukuwa sawa kimtizamo.

"...Israel ilipoiteka ardhi ya Kiarabu, pamoja na Palestina mwaka 1967, Baba wa Taifa Mwl. Julias Nyerere alikemeasema; “The establishment of the state of Israel was an act of aggression against the Arab people…Israel must evacuate the areas … - without exception- ...we cannot condone aggression on any pretext, nor accept victory in war as a justification for the exploitation of other lands, or government over other peoples.“Huu ndio uliokuwa msimamo wa TZ 1967. Tulivunja uhusiano na Israel, na tulikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuipokea ubalozi wa Palestina." Alisema Pref. Sheriff akihoji ukimya wa sasa.

Waandaaji wa mkutano huo pia walitangaza kufanya maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Quds Duniani yanayotarajiwa kufanyika Julai 25, 2014; kwa Tanzania maandamano yataanzia Ilala Boma jijini Dar es Salaam kwenda Uwanja wa Kigogo na baadaye Karimjee ambapo kutakuwa na mada anuai.
Kanali Mstaafu Iddi Kipingu wa tatu kushoto akikabizi misaada ya vyakura kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Daru-Alqm cha yombo misaada iliyotolewa na Timber Land Jogging and Sports Club.
Baadhi ya wtoto wakifuturu wakati wa futari iliyoandaliwa na klub ya jogging ya timber land iliyopo yombo kilakala
Baadhi ya kina mama na watoto nao wakipata futari
BAADHI YA WANACHAMA WANAWAKE WA KLUB YA TIMBER LAND YA YOMBO KILAKALA WAKIPATA FUTARI YA PAMOJA
Mlezi wa klabu ya Timber land sports club ya yombo kilakala , bi Carren-Flora Mgonja wa pili kushoto akiwa na baadhi ya wanachama mara baada ya kumaliza futari.
Mlezi wa klabu ya Timber land sports club ya yombo kilakala , bi. Carren-Flora Mgonja  akizungumza wakati wa futari hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Timber Land Chorai JAohn akizungumza.
Kanali Mstaafu Iddi Kipinguakitoa nasaha zake.
Diwani wa kata ya yombo kilakala bi, Elizabeth Magwaja akiongea.
Kanali Mstaafu Iddi Kipingu akikabidhiwa cheti cha ushiriki wake.