Moja ya kichwa cha binadamu kilichotolewa kwenye mifuko hiyo.
Miguu iliyokaushwa ikiwa kwenye mifuko. Picha kwa hisani ya Daresalaam-yetu.blogspot 
Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika  mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
HABARI ZA AWALI TOKA KWA MASHUHUDA WA TUKIO:
Habari zilizotufikia usiku wa leo Julai 21, 2014 maeneo ya Bunju B jijini Dar es Salaam watu wawili ambao walikuwa na gari dogo aina ya Isuzu wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakiwa viungo vya binadamu ambayo walikuwa wamevifunga katika mifuko ya plastiki.

Mashuhuda waliokuwa eneo la tukio walisema waliona gari aina ya Isuzu ikiwa imesheheni viungo mbalimbali vya binadam ikiwemo miguu, mikono, vichwa n.k.Viungo hivyo vilikua ni vibichi na vinavuja damu na vilikuwa vinaenda kutupwa damp la Mpiji..

Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa dereva wa gari hilo alifanikiwa kumwaga viungo safari ya kwanza (Trip) eneo la shule ya Consolata ya Masista na aliporudi kumwaga awamu ya pili ndipo wananchi walipowaita polisi na kufanikiwa kumkamata dereva huyo.

Polisi wa Kituo cha Bunju A na Wazo waliamua kupiga risasi hewani ili kuweza kuwatawanya watu waliovamia Kituo cha Polisi Bunju A wakiwa na lengo la kumuua dereva aliyekamatwa akiendesha gari hilo lililokuwa limejaa viungo hivyo.

Endelea kufuatilia sakata hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

2 comments:

  1. Dunia binadamu hamumuogopi muumba wenu tena??!! Kitendo hik cha kutoa uhai wa binadamu mwenzioi ni cha kinyama na kinapaswa kulaaniwa na kila kiumbe chenye uhai!!

    ReplyDelete
  2. Jaman hivi hawa imtu wafanywe nn mmejivunjia heshima ynu sasa.

    ReplyDelete