Ilikuwa mnamo Julai 20, 2014 mara baada ya kumaliza sherehe za harusi katika ukumbi wa JKT MGULANI jijini Dar es Salaam nikatembea kwa mguu hadi kituo cha daladala, nilipofika kituoni ikapita haice na waliponiona konda akasema unaenda wapi nikamjibu Kariakoo, basi nikafunguliwa mlango na kuingia na kukaa kwenye siti na kulikuwa kuna abiria saba.

Mara baada ya kuwa nimekaa nikasikia sauti nikiambiwa oya tupo kazini hapa toa vyetu, mimi nikajua nauli nikatoa shilingi mia tano ili nilipe, mara nikatolewa panga na mwingine akatoa bastola na kusema nitoe fedha zote nilizonazo na niwape simu, kiukweli nilikuwa sina jinsi kabisa kwani nilikuwa kwenye kumi na nane zao.

Nikawapa simu na vijihela nilivyo navyo na wakanisachi ili kuhakikisha kuwa hawaniachi hata na senti moja, waliporidhika wakasimamisha gari, ila mmoja akasema si tumpe hata alama kidogo, basi wakati huo nilimwomba Mungu na kwa bahati nzuri wakanishusha na wakaondoka zao, kwa kuwa sikuwa na fedha tena basi nikatembea tu kurudi nyumbani.

Pole sana Deo Julius kwa tukio hili lililokukuta.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: