Wananchi waliofika eneo la tukio wakijaribu kuweka kumbukumbu....
 Moja ya mguu ulikokuwa kwenye mfuko huo.
Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanane kuhusiana na tukio la kuokotwa viungo vya binadamu katika eneo la Bunju A jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa watu wanane wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Kova amesema kuwa jopo la Wataalamu saba limeundwa kuchunguza tukio hilo na amethibitisha kuwa viungo vile vilikuwa ni vya maiti,ambavyo hutumika na madaktari kwa elimu ya matibabu na utafiti.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: