Na Mwandishi Wetu -Narok, Kenya.

Rais wa Kenya, William Ruto, amempongeza mwanasiasa David Keter maarufu kama Dollarline kwa kushinda katika kura za mchujo za chama cha United Democratic Alliance (UDA) katika Jimbo la Emurua Dikirr Constituency.

Kupitia ujumbe wake, Rais Ruto alimpa pongezi Keter kufuatia ushindi huo muhimu uliompa tiketi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo ujao wa jimbo hilo.

Aidha, Rais Ruto alimpongeza pia mpinzani wake Bernard Ng'eno maarufu kama Buluu kwa kuendesha kampeni imara, akieleza kuwa ushindani huo umeimarisha misingi ya demokrasia ndani ya chama hicho kuanzia ngazi za chini.

“Tunapongeza ushindani wa haki na wa kidemokrasia uliofanyika, ambao unaimarisha chama chetu na kuonesha mshikamano wa wanachama,” ilieleza sehemu ya ujumbe wa Rais Ruto.

Rais huyo alisisitiza kuwa baada ya mchakato wa mchujo kukamilika, ni muhimu kwa wanachama wote wa UDA kuungana na kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa ili kuhakikisha ushindi katika uchaguzi mdogo.

“Tunakwenda mbele kama timu moja imara, tukiwa tumeungana nyuma ya mgombea wetu na ajenda ya chama,” aliongeza.

Ushindi wa Keter unatarajiwa kuongeza ushindani mkali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, huku chama cha UDA kikilenga kuimarisha nafasi yake kisiasa katika Kaunti ya Narok na maeneo ya jirani.

Moshi ilichangamka kwa mara nyingine tena huku maelfu ya wakimbiaji, mashabiki, na watazamaji wakikusanyika kwa toleo la mwaka 2026 la Kilimanjaro Marathon. Kilichoanza zaidi ya miongo miwili iliyopita kama mbio, kimekua na kuwa moja ya majukwaa yenye nguvu zaidi kitaifa nchini Tanzania, yakileta pamoja michezo, utalii, utamaduni, na jamii kwa namna ya kipekee.

Mbio za mwaka huu zilivutia ushiriki mkubwa kutoka kote Tanzania na duniani kwa ujumla, na kuimarisha nafasi yake kama tukio muhimu la utalii wa michezo. Kuanzia wanariadha wa kiwango cha juu hadi wakimbiaji wa mara ya kwanza, tukio hili liliunda uzoefu wa pamoja uliovuka mstari wa mwisho wa mashindano. Haikuwa tu kuhusu ushindani, bali pia ushiriki, muunganiko, na fahari ya taifa.

Kiini cha mafanikio haya ya muda mrefu ni Tanzania Breweries Public Limited Company kupitia chapa yake kuu ya Kilimanjaro Lager, ambayo imekuwa ikiunga mkono mbio hizi kwa miaka mingi. Ushirikiano huu umechukua nafasi kubwa katika kuunda tukio hili kuwa jukwaa linalotoa thamani ya kijamii na kiuchumi.

Mbio hizi zinaendelea kuleta faida halisi kwa uchumi wa eneo husika. Hoteli zilijaa wageni, huduma za usafiri ziliongezeka, na wafanyabiashara wadogo walipata ongezeko la biashara kutokana na wageni waliokuja Moshi. Kwa biashara nyingi ndogo, wiki ya marathon ni mojawapo ya vipindi muhimu zaidi kwa mwaka. Faida hii inaonesha mchango wa tukio hili katika kusaidia maisha ya watu na kuimarisha uchumi wa ndani.
Zaidi ya shughuli za kiuchumi, marathon hii inaongeza mwonekano wa Tanzania kimataifa. Washiriki wa kimataifa na vyombo vya habari vinaendelea kuiweka Tanzania kama kivutio kinachotoa si tu uzuri wa asili bali pia uzoefu wa kiwango cha kimataifa uliopangwa vizuri. Mkoa wa Kilimanjaro hasa unafaidika na mwonekano huu, ukithibitisha nafasi yake kama kitovu cha utalii na burudani za kipekee.

Kampeni ya mwaka huu, “The Best of Us - Vyakwetu Vizuri,” iliongeza maana ya kina kwa tukio hili. Ikitokana na misemo, methali, na lugha ya kila siku ya Watanzania, kampeni hii ilisherehekea utambulisho, uthabiti, na maadili kwa pamoja. Iliunganisha chachu ya mbio na maisha halisi ya Watanzania, na kufanya marathon hii kuwa ya kibinafsi na ya kitaifa kwa wakati mmoja.

Afya na ustawi pia vinaendelea kuwa sehemu muhimu ya faida ya marathon hii. Kwa miaka mingi, tukio hili limechangia kujenga utamaduni wa kukimbia na kuishi maisha yenye afya nchini. Watu wengi zaidi wanashiriki katika shughuli za mazoezi, na taasisi mbalimbali zinaanzisha majukwaa yanayohamasisha harakati na ustawi wa mwili. Marathon imekuwa mfano wa kile ambacho juhudi endelevu za afya ya jamii zinaweza kufanikisha nchini Tanzania.

Burudani haikuishia kwenye mbio pekee. Kili Dome kwa mara nyingine ilileta pamoja michezo, muziki, sherehe, na kuunda mazingira yenye hamasa ambapo washiriki na watazamaji waliweza kuungana na kujiburudisha. Mchanganyiko huu wa michezo na maisha ya kijamii unaakisi nafasi pana ya marathon katika kuunda uzoefu wa pamoja.

Akizungumza baada ya tukio, Mkurugenzi Mtendaji Michelle Kilpin alieleza ukuaji na umuhimu unaoendelea wa marathon hii kama jukwaa la kitaifa.

“Marathon ya Kilimanjaro inaendelea kuwaleta watu pamoja kutoka asili mbalimbali kwa namna inayoakisi maana halisi ya Tanzania. Inaunga mkono utalii, inakuza afya, na inajenga mahusiano yenye maana katika jamii. Tunajivunia kuona jinsi tukio hili linavyoendelea kukua na kutoa thamani zaidi ya mbio zenyewe.”

Kadri toleo la mwaka 2026 linavyohitimishwa, Kilimanjaro Marathon inabaki kuwa zaidi ya tukio la kila mwaka la michezo. Ni jukwaa linalochochea shughuli za kiuchumi, linaimarisha mshikamano wa jamii, linahamasisha maisha yenye afya, na linaonesha Tanzania kwa dunia.

Kupitia uungwaji mkono wake unaoendelea, Tanzania Breweries Plc kupitia Kilimanjaro Lager inaendeleza dhamira yake ya kusaidia mipango inayowaunganisha watu na kuchangia maendeleo ya muda mrefu ya taifa. Mbio zinaweza kuishia kwenye mstari wa mwisho, lakini faida yake inaendelea kwa muda mrefu zaidi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.


Mhe. Lukuvi amefariki dunia tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkoani Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa George Masaju akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano, Hayati John Pombe Magufuli... Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa Balozi Moses Kusiluka akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali wa kitaifa na serikali wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Karimjee Hall kushiriki ibada ya kumuombea na kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi, huku wakisaini kitabu cha maombolezo kuonesha heshima zao za mwisho.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, aliyesaini kitabu hicho akiambatana na mkewe Salma Kikwete, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mchinga.

Pia, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, alijitokeza na kusaini kitabu hicho, akifuatiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba.

Wengine waliotoa heshima zao ni pamoja na Mama Anna Mkapa, Jaji Mkuu wa Tanzania George Masaju, pamoja na Mama Janeth Magufuli.

Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi Moses Kusiluka, Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jacob Mkunda, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari, nao walifika na kusaini kitabu cha maombolezo.

Ibada hiyo imefanyika leo Machi 28, 2026, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kitaifa za kuaga mwili wa kiongozi huyo aliyefariki dunia Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.

Katika salamu zao, viongozi hao walimwelezea marehemu Lukuvi kama kiongozi aliyekuwa na mchango mkubwa katika utumishi wa umma, hususan katika kusimamia sera na uratibu wa shughuli za serikali pamoja na kutetea maslahi ya watu wenye ulemavu.

Umati mkubwa wa wananchi nao umejitokeza kushiriki katika maombolezo hayo, wakionesha upendo na heshima kwa kiongozi huyo aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.

Ratiba ya mazishi inaendelea kuratibiwa na serikali, huku Watanzania wakiendelea kuomboleza kifo cha mmoja wa viongozi waliotumikia taifa kwa muda mrefu.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Msanii wa muziki wa hip hop nchini, Wakazi (Webiro Wasira), ameanza rasmi mchakato wa kisheria kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyomkuta na hatia ya kusambaza taarifa za uongo dhidi ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Baba Levo (Clayton Chipando).

Katika hukumu hiyo, mahakama ilimuamuru Wakazi kulipa fidia ya shilingi milioni 100 pamoja na kumuomba radhi Baba Levo na kukanusha taarifa alizodaiwa kusambaza kupitia mitandao ya kijamii, blogu na YouTube.

Hata hivyo, kupitia taarifa yake kwa umma, Wakazi amesema ameridhia kupeleka shauri hilo mahakamani kupinga uamuzi huo, akidai kuwa hukumu ilitolewa upande mmoja (ex parte) bila yeye kushirikishwa ipasavyo katika mchakato wa usikilizwaji wa kesi.

Ameeleza kuwa tayari amemkabidhi jukumu hilo wakili wake, Peter Kibatala, ambaye ameanza mchakato wa dharura wa kuwasilisha maombi ya kutengua hukumu hiyo ili apewe nafasi ya kusikilizwa.

“Masuala haya yako mikononi mwa wakili wangu, na tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa chini ya utaratibu wa dharura,” imeeleza sehemu ya taarifa ya Wakazi.

Chanzo cha Mgogoro

Mgogoro kati ya wawili hao ulianza baada ya Baba Levo kupoteza begi lenye simu alipokuwa safarini nchini Uturuki. Kufuatia tukio hilo, Wakazi alidai kupitia mitandao ya kijamii kuwa Baba Levo alihusika na wizi wa simu za watu nchini Marekani, madai ambayo baadaye yalikanushwa.

Kwa mujibu wa Baba Levo, uwanja wa ndege wa Istanbul Airport ulimtaarifu kuwa begi lake lilikuwa limepatikana likiwa na vifaa vyote, jambo lililothibitisha kuwa hakukuwa na tukio la wizi kama ilivyodaiwa.

Baada ya hapo, Baba Levo alichukua hatua za kisheria kupinga madai hayo kwa madai ya kuchafuliwa jina, na kesi hiyo kusikilizwa hadi kufikia hukumu iliyotolewa.

Hatua za Sasa

Kwa sasa, Wakazi anapinga hukumu hiyo akisisitiza kuwa hakupatiwa haki ya kusikilizwa kabla ya uamuzi kutolewa. Amesisitiza kuwa hatatoa maoni zaidi hadharani kutokana na unyeti wa suala hilo na kwamba taarifa rasmi zitatolewa na wakili wake kulingana na taratibu za taaluma ya sheria.

Kwa upande mwingine, hukumu ya awali inaendelea kuzua mjadala miongoni mwa wananchi na wadau wa mitandao ya kijamii kuhusu uwajibikaji wa maudhui yanayosambazwa mtandaoni na athari zake kisheria.

Hatua ya Wakazi kupinga hukumu hiyo sasa inaweka wazi kuwa sakata hilo bado halijafungwa rasmi, huku macho ya wengi yakielekezwa kwenye uamuzi wa mahakama kuhusu maombi ya kutengua hukumu hiyo.

Na Mwandishi Wetu.

Dar es Salaam — Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa adhabu mbalimbali kwa klabu na waamuzi kufuatia matukio ya kinidhamu yaliyojitokeza katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC, ikiwemo kuifungia mchezaji wa Young Africans, Djigui Diarra, na kuipiga faini klabu ya Simba SC.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TPLB, Diarra amefungiwa mechi tatu pamoja na kutozwa faini ya Sh milioni 2 baada ya kumshambulia mwamuzi kufuatia mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Young Africans uliomalizika kwa sare ya 1-1 katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Aidha, mchezaji huyo pia ametozwa faini nyingine ya Sh milioni 2 kwa kosa la kuonesha ishara isiyo ya kiungwana kwa mwamuzi baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Katika hatua nyingine, klabu ya Simba SC imetozwa faini ya Sh milioni 10 baada ya mashabiki wake kuwarushia waamuzi chupa za maji walipokuwa wakitoka uwanjani kufuatia mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC uliomalizika kwa sare ya 1-1. Tukio hilo limetajwa kuwa ni la kujirudia ndani ya kipindi kifupi.

Kwa upande wa klabu ya TRA United, nayo imetozwa faini ya Sh laki tano baada ya wachezaji wake kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mchezo mmoja dhidi ya Young Africans, hali inayokiuka kanuni za nidhamu za ligi.

Sambamba na adhabu hizo, TPLB pia imewachukulia hatua baadhi ya waamuzi wa mechi husika. Mwamuzi wa kati, Gilbert Mrina, ameshushwa daraja kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kwa kosa la kinidhamu lililofanywa na mchezaji Diarra, huku mwamuzi msaidizi Abdulaziz Ally akifungiwa mechi tano kwa kushindwa kutafsiri vyema sheria ya mpira wa miguu katika tukio la kuotea.

TPLB imesisitiza kuwa hatua hizo zimechukuliwa kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ili kuhakikisha nidhamu, haki na uwazi vinaendelea kudumishwa katika mashindano hayo.

• Ni muuza wa kuni, maji na viazi aliyeshinda boda boda ya PigaBet

Dar es Salaam — Kuna watu wanaotafuta kazi. Halafu kuna watu ambao kila siku wanajitengenezea kazi kutoka kila pembe ya maisha. Muhammad Mussa wa Mburahati Motomoto ni mmoja wao.

Akiwa na miaka 45, mke na watoto wawili, Muhammad si mtu wa kukaa. Ana bucha la kuni, anauza maji, na pia anasambaza viazi vya chipsi kwenye magenge na sehemu za kukaanga chipsi. Kwa kifupi, maisha yake yanatembea kwenye biashara zaidi ya moja. Tatizo lilikuwa moja tu: mwendo wa kuzifikisha hizo biashara kwa watu.

Kutoka jirani na Soko la Mabibo hadi kwa wateja wake, usafiri ulikuwa ukikata kasi ya kazi. Hapo ndipo ushindi wake wa boda boda kupitia kampeni ya #ShindaBoda ya PigaBet unapopata maana ya kweli.

Mohammed anasema boda hiyo itakuwa msaada mkubwa katika biashara zake za kila siku, hasa kwenye kubeba na kusambaza bidhaa zake kwa urahisi zaidi.

“Itanisaidia katika shughuli zangu za kibiashara. Nitaanza kuongeza kipato na kufanya biashara nyingine,” amesema Mohammed.
Kwa maelezo yake, boda hiyo itarahisisha kubeba magunia ya viazi kutoka soko la Mabibo na kuyapeleka kwenye sehemu za kukaanga chipsi, pamoja na kusambaza kuni kwenye maeneo mbalimbali.

Kwa mtu anayesimamia biashara zaidi ya moja, hiki si chombo cha kutembelea tu. Hiki ni kifaa cha kazi.

Mohammed anaamini ushindi huu utaongeza ufanisi wa biashara zake na kusaidia kuimarisha maisha ya familia yake. Kile alichoshinda si usafiri tu, bali ni nafasi ya kusogeza biashara zake mbele kwa mwendo mmoja.

Kwa Mohammed, huu si ushindi wa kutazamwa. Ni mwendo wa kusukuma maisha.
18+ | Cheza kwa uwajibikaji.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, akimvalisha Cheo cha Kamishna wa Polisi (CP) Alex S. Mkama, baada ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kumpandisha cheo kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kuwa Kamishna wa Polisi (CP) na kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Jamii, hafla ya kumuapisha imefanyika Machi 26, 2026 Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.