Articles by "UJUMBE WA JUMAPILI"
Showing posts with label UJUMBE WA JUMAPILI. Show all posts

Mimina Neema. Ni Toleo la 11 la Kwaya ya Mtakatifu Kizito, Parokia ya mwenye heri Anuarite - Makuburi, Dar es salaam. Huu ni wimbo mmoja miongoni mwa nyimbo 12 zinazofanya Album hii. 
Na Mwl Christopher Mwakasege.

Jina la Yesu Kristo litukuzwe milele!

Leo nataka kuanza mfululizo mwingine wa somo, ambao naamini utakuwa wa msaada sana kwako, katika kuimarisha uhusiano wako na Mungu.

Somo lenyewe ni hili: “ROHO MTAKATIFU ANAVYOONGOZA WANA WA MUNGU KUTEMBEA NA MUNGU KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MAISHA YAO”.

Mfano na 1: Tunaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume 27:10, tunaona jinsi mtume Paulo alivyoarifiwa na Roho Mtakatifu, juu ya hatari iliyokuwa mbele yake, katika safari aliyokuwa nayo na wenzake.

Mtume Paulo akawaambia wenzake hivi: “naona kwamba safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi si ya shehena na marikebu tu, ila na ya maisha yetu pia”. Na jambo hili likatokea kweli kama alivyosema!

Swali la msingi la kujiuliza hapa ni kutaka kujua mtume Paulo alijuaje juu ya hatari ile! Roho Mtakatifu alitumia njia gani kumjulisha kwa uwazi namna ile? Je, na sisi leo Roho Mtakatifu anaweza kutujulisha juu ya hatari zilizo mbele yetu na tukauelewa ujumbe wake?

Mfano na 2: Je! Unafahamu mtume Paulo na wenzake walikuwa wanaamuaje juu ya eneo la kwenda kupeleka neno la Mungu? Ukisoma habari zao kwenye biblia, utajua ya kuwa ni kwa msaada wa uongozi wa Roho Mtakatifu.

Kuna wakati walikuwa wakipita nchi za Frigia na Galatia zilizokuwa Asia, wakitaka kulihubiri neno la Mungu huko. Biblia inasema walikatazwa “na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia” (Matendo ya Mitume 16:6).

Biblia inaendelea kutueleza juu ya safari yao hiyo ya kwamba: “Walipofika kukabili Misia wakajaribu kwenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa” (Matendo ya Mitume 16:7). Na baada ya hapo, Roho akawapa kufahamu kuwa, walitakiwa kwenda Makedonia kuhubiri neno huko. Na ndivyo walivyofanya!

Swali la msingi la kujiuliza hapa, ni kutaka kujua walijuaje kuwa katika wazo walilokuwa nalo, Roho Mtakatifu alikuwa anawakataza wasilifanye, au anawanyima ruhusa wasilifanye? Na ikiwa Roho Mtakatifu ana wazo analotaka walitekeleze walilijuaje?

Je! Kwetu sisi – tulio wana wa Mungu kipindi hiki, tunaweza kupata msaada wa Roho Mtakatifu kuhusu mahali pa kwenda, au mahali pa kutokwenda, kama akina mtume Paulo walivyosaidiwa?

Na ikiwa ni hivyo – ina maana si suala la mtoto wa Mungu kuamua kwenda mahali popote atakavyo, bali hili ni muhimu ajue wazo la Roho Mtakatifu aliye naye ndani yake kuhusu safari yake hiyo!

Mfano na. 3: Roho Mtakatifu ndiye aliyemsaidia Yesu kuchagua wanafunzi wake kumi na wawili. Biblia inasema habari hizi za Yesu ya kuwa: “Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume” (Luka 6:12,13).

Habari hii haituambii moja kwa moja ni kwa namna gani, na kwa njia gani Yesu aliweza kufanya maamuzi ya nani amchague, na nani asimchague “miongoni” mwa wanafunzi wengi aliokuwa nao wakati ule!

Kwa msomaji yeyote wa biblia, anajua ni Roho Mtakatifu aliyemsaidia kufanya uchaguzi wa watu wa kukaa naye karibu! Lakini swali la kujiuliza ni kutaka kujua Roho Mtakatifu alimsaidia kwa njia zipi?

Nina uhakika tukijua jinsi Yesu alivyosaidiwa katika hili, itakuwa ni rahisi kwetu kusaidiwa na Roho Mtakatifu kujua watu wa kuwa nao karibu, na watu wa kukaa nao mbali! Pia naamini tunaweza kujua ni nani wa kushirikiana naye, na ni nani wa kutoshirikiana naye!

Biblia inasema katika Warumi 8:24 tunasoma ya kwamba: “wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu”.

Na Yesu akizungumza juu ya Roho Mtakatifu atakapokuja kwenye maisha ya wanafunzi wake alisema: “Lakini yeye atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote;…na mambo yajayo atawapasha habari yake” (Yohana 16:13).

Nataka ujue ya kuwa, ikiwa wewe ni mtoto au mwana wa Mungu, ni haki yako itokayo kwa Baba yako, yaani Mungu, kuongozwa na kutegemea kuongozwa na Roho Mtakatifu!

Uwe mtumishi wa Mungu au usiwe mtumishi wa Mungu – ili mradi tu wewe ni mtoto wa Mungu; Roho Mtakatifu uliye naye amepewa jukumu la kukusaidia, ikiwa ni pamoja na jukumu la kukuongoza katika maisha yako ya kila siku!

Ndani ya mfululizo wa somo hili, tutajifunza njia kadhaa anazotumia Roho Mtakatifu kumwongoza mwana wa Mungu. Kwa hiyo nakuombea kwa Mungu, akuwezeshe kukaa mkao wa kujifunza somo hili!
Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka sahihi hati ya kiapo baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo leo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka wakfu na kusimikwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Dkt Jacob Chimeledya kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Willim Mkapa akimpongeza Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Jaji Mkuu wa Tanzania Mstaafu Mhe Augustino Ramadhani akipiga kinanda kwenye sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es Salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama janeth Magufuli wakikomunika kwenye sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama janeth Magufuli pamoja na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakishiriki katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea machache baada ya kushiriki katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsihi Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob Chimeledya kuketi kwenya kiti alichoandaliwa yeye wakati wa kupiga picha za pamoja wakati wa sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob Chimeledya na viongozi wengine wakati wa sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018

Picha na IKULU.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Tehama kwenye mradi wa PS3 Desderia Wengaa akitoa maelezo ya Utangulizi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Planrep na FFARS.
Baadhi ya washiriki kutoka Mikoa mitano ya Tanga, Tabora, Manyara, Singida na Dodoma wakati wa mafunzo ya Planrep na FFARS.
Erick Kitali Mkurugenzi wa TEHAMA, OR-TAMISEMI akielezea kwa ufupi mifumo iliyoboreshwa ya Planrep na FFARS wakati wa mafunzo yanaendelea Mkoani Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dododma Rehema Madenge akifungua mafunzo ya siku nane kwa wataalamu wa Afya, Mipango na Fedha kutoka Mikoa Mitano chini ya ufadhili wa mradi wa Uimarishaji Mifumo (PS3).
Pichani ni Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge (Katikati mbele) akiwa na wakufunzi wa mafunzo hayo.(Picha zote na Ofisi ya Rais TAMISEMI)
---
Serikali mkoani hapa imesema ili mpango wa PlanRep uweze kufanikiwa kwa ufasaha hakuna budi kuzijumuisha idara za Elimu katika mafunzo yanayoendelea mkoani Dodoma yanayo wajumuisha wataalam wa mipango pamoja na afya kutoka mikoa mitano ya Tanga, Tabora, Manyara, Singida na wenyeji Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya bajeti kwakutumia mfumo mpya wa PlanRep na FFARS.

Akifungua mafunzo ya siku nane mkoani hapa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge, amesema moja ya vitu vilivyokuwa vikikwamisha masuala ya bajeti ni pamoja na kutokuwa na takwimu sahihi huku akinyooshea kidole takwimu za idara za elimu.

“Ninatamani sana takwimu za elimu ziwe sahihi hasa katika uwasilishaji wa taarifa za mitihani ili ziweze kuendana na idadi ya wanafunzi na fedha zinazo ombwa, kuepusha madudu yanayo wasilishwa” alisema madange na kuongeza kuwa katika sekta ya elimu ndipo kuna sarakasi ambazo hata mruka sarakasi mwenyewe hata yeye hamjui.

Madenge ambaye kwa taaluma ni Mchumi na aliyeshughulika na kuratibu shughuli za bajeti kwa muda mrefu, amesema ili mipango iweze kuendana na mahitaji suala la kuwa na takwimu sahihi haliepukiki na kuamini kuwa chini ya PlanRep mpya itakuwa mwarobaini katika kutatua changamoto hizo.

Madenge amesema mfumo wa PlanRep ulioboreshwa pia unaenda kutumika kuanzia ngazi ya msingi yaani vituo vyetu vya kutolea huduma ambapo utawezesha kuandaa mipango na bajeti kutokana na vipaumbele na mahitaji ya wananchi ambao ndio waathirika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mifumo ya TEHAMA wa PS3, Desderi Wangaa, amesema, PlanRep mpya iliyoboreshwa imefanyia kazi changamoto kwa kuhakikisha kwamba mipango na bajeti unaingizwa kwa kila mtoa huduma, na unaingiza namba za utambulisho kwa kila mtoa huduma mmoja mmoja kwa kila sekta lakini pia mfumo huu umeweka nafasi ya kila mtoa huduma kuainisha matokeo yanayotegemewa (Service Outputs).

Awali akitoa maelezo ya utangulizi, Mkurugenzi wa TEHAMA wa OR-TAMISEMI, Erick Kitali, alisema mfumo umezingatia mahitaji ya idara zote za mamlaka za serikali za mitaa na ambao ni fungamanifu unaotumia muda mfupi kukamilisha kazi za uratibu wa bajeti na taarifa za hesabu toka vituo vya huduma.

“Kutokana na kuwa fungamanifu hatutegemei kuona Serikali za Mitaa zikikwama katika uandaaji wa bajeti, na tuna uhakika na ufanisi wa hali ya juu katika kazi hii usahihi unaotakiwa” alisema Erick na kuongeza (Efficient and Effective).

Awali akimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa, Mkurugenzi wa mamalaka za serikali za Mitaa Beatrice Kimoleta, alisema kuwa na mfumo ni jambo moja na utendaji ni suala linguine hivyo suala la kujituma katika kuhakikisha mifumo inafanya kazi vema kila mmoja lazima awiwe katika utendaji wake.

“Tulitumia muda mwingi katika kuandaa bajeti na muda mfupi ukatumika katika kusimamia lakini katika PlanRep hii mpya mtaona muda wa uandaaji bajeti utakuwa utakuwa mfupi na muda mwingi utatumika katika suala la ufatiliaji na usimamizi”. Rai yangu niwasihi sote tuwe makini wakati wote wa mafunzo ili tukitoka hapa basi mipango yetu iwe yenye kuzingatia mahitaji.

PS3 kwakushirikiana na OR-TAMISEMI tayari wametoa mafunzo kwa mikoa na Halmashauri zote nchini na katika awamu hii ya mwisho inahusisha wataalamu kutoka mikoa ya Tanga, Tabora, Singida Manyara na Dodoma ambayo ni mwenyeji.

Aidha uzinduzi wa PlanRep mpya utafanyika 5 Septemba, 2017 na Mgeni Rasmi anatazamiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassimu Majaliwa (MB).
Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Moses Kombe (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuambwa msalabani kwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo jioni.
Igizo likiendelea.
Askofu mstaafu Dk. Alex Malasusa akisalimiana na waumini wa kanisa hilo baada ya ibada ya Ijumaa Kuu.
Muonekano wa waumini wakati wa ibada hiyo.
Kwaya Kuu ya Ushairika huo ikitoa burudani ya nyimbo za kifo chake Yesu Kristo wakati wa kuhitimisha ibada hiyo.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa nje kwa kuhitimisha ibada hiyo.
Waumini wakitakiana kheri ya Ijumaa Kuu baada ya ibada hiyo.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea machache alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru (kushoto) na Fr. Asis Sylvester Mendoca (wa pili kulia) wakimsikiliza Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke, akiongea kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
 Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa akiongoza sala wakati wa hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe. Kushoto ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli. Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na masista alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe,, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na waumini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, Fr. Asis Sylvester Mendoca baada ya kuhitimisha hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.
Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
---
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo April 2, 2017 ameungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.

Kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rigambwa na kuongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mama Magufuli amemtakia kila la heri Fr. Kaombwe katika kituo kipya cha kazi, na pia amempa salamu toka kwa Rais John Pombe Magufuli ambaye naye amemtakia heri na fanaka kwa uhamisho huo.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa alimpongeza Fr. Kaombwe kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akihudumu katika Paroko hiyo kwa takriban miaka mitatu na nusu, na pia alitumia nafasi hiyo kumtambulisha Fr. Asis Sylvester Mendoca ambaye atakaimu nafasi ya Fr. Kaombwe.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, amempongeza Fr. Kaombwe kwa mambo mengi aliyoyafanya kanisani hapo, na kwa niaba ya jumuiya ametoa shukurani nyingi kwa huduma alizokuwa akiwapatia.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mhe. Edward Lowassa akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha katika misa maalamu ya mwaka mpya 2017 ambapo amewataka watanzania wote bila kujali itikadi zao kufanya kazi kwa bidii.

Mh Lowassa ameshiriki ibada hiyo akiambatana na familia yake pamoja na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali Mkoani Arusha na Jimbo la Monduli wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mhe. Isack Joseph , Wakili John Mallya na viongozi wengine.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa, mama Regina Lowassa akisalimiana na mchungaji wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha Laison Saning'o katika Ibada maalamu ya mwaka mpya 2017.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akisalimiana na mchungaji wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha Laison Saning'o katika Ibada maalamu ya mwaka mpya 2017.
Wakili John Mallya (aliyeshika biblia) akisoma neno kwenye biblia katika Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha katika misa maalamu ya mwaka mpya 2017.
Mtoto mkubwa wa Mh Lowassa, Fred Lowassa (mwenye shati jeupe) akiwa na waumini wengine katika Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha leo.
Mtoto mkubwa wa Mh Lowassa, Fred Lowassa (mwenye shati jeupe) akiwa na waumini wengine katika Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha leo.
Mchungaji  Bruno Mwakibolwa kutoka Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Temeke Jijini Dar es salaam, jumapili iliyopita Oktoba 16, 2016 alihudumu katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, baada ya kuwasili katika kanisa hilo akitokea nchini Kenya.

Ilikuwa Ibada iliyojaa neema ambapo Mchungaji Mwakibolwa aliwahimiza waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya kumtumia Mungu kwa moyo wa kweli na watabarikiwa maishani mwao.

Alisema ziko njia mbalimbali za kumtumikia Mungu ikiwemo kuhakikisha waumini wanajikita katika kumjengea Mungu Makanisa bora ili kuwezesha neno la Mungu kusonga mbele.

Na BMG
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza
Mama Mchungaji, Mercy Daniel Kulola, akiwa katika ibada hiyo
Kiongozi wa timu ya kusifu na kuabudu, EAGT Lumala Mpya akihudumu katika ibada hiyo
Waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza wakiwa kwenye ibada hiyo
Waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza wakiwa kwenye ibada hiyo
Hii pia ni miongoni mwa njia bora kumtumikia Mungu
Kutoka kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Jijini Dar es salaam, Bruno Mwakibolwa, Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola pamoja na Mama Mchungaji, Mercy Daniel Kulola.
Mmoja wa waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza akiwa kwenye ibada hiyo
Waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza wakiwa kwenye ibada hiyo.