Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama wakiwa katika picha ya pamoja na Raila Odinga na Mama Ida Odinga, tukio lililodhihirisha ukaribu wa kifamilia na uhusiano wa kihistoria kati ya familia hizo mbili.

Na Mwandishi Wetu

Marekani – Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama, ameungana na Wakenya na jumuiya ya kimataifa kuomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo Odinga, akimtaja kama shujaa wa kweli wa demokrasia.

Katika salamu zake za rambirambi, Obama alisema Raila alikuwa kiongozi wa kizazi cha pekee, ambaye maisha yake yote aliyatumia kupigania haki, uhuru na kujenga msingi wa utawala wa kidemokrasia nchini Kenya.

“Raila Odinga was a true champion of democracy. A child of independence, he endured decades of struggle and sacrifice for the broader cause of freedom and self-governance in Kenya. Time and again, I personally saw him put the interests of his country ahead of his own ambitions,” alisema Obama.

Akimrejelea Raila kama kiongozi aliyejitolea bila kuyumbishwa, Obama alisema mara nyingi alimshuhudia akitanguliza masilahi ya taifa badala ya faida binafsi, jambo ambalo limeacha alama ya kudumu katika historia ya Kenya.

Obama aliongeza kuwa tofauti na viongozi wengi duniani, Raila alikuwa tayari kuchagua njia ya maridhiano ya amani bila kusaliti misingi na thamani zake za msingi.

“Like few other leaders anywhere, he was willing to choose the path of peaceful reconciliation without compromising his core values,” alisisitiza.

Kauli ya Obama imeongeza uzito wa heshima na hadhi ambayo Raila Odinga anaendelea kupewa ndani na nje ya Kenya, ambapo viongozi wa mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria mazishi yake yanayopangwa kufanyika Jumapili, Oktoba 19, 2025, nyumbani kwake Bondo, Kaunti ya Siaya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: