Bukoba, Septemba 29, 2025: Viongozi wa Serikali, Kanisa na waumini wa Kanisa Katoliki leo wamejitokeza kwa wingi kuaga mwili wa Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyekuwa Balozi wa Baba Mtakatifu, kupitia Misa Takatifu ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki la Jimbo la Bukoba, mkoani Kagera.

Misa hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Kardinali Protase Rugambwa, ambapo pia walihudhuria Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa.

Viongozi wengine walioungana na waumini ni pamoja na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Wolgang Pisa; Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Angelo Acattino; Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Mhashamu Jovitus Mwijage; pamoja na viongozi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha.
Waamini, Mapadri na Watawa kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Kagera pia walihudhuria ibada hiyo maalum ya kumuaga kiongozi huyo wa Kanisa.

Hayati Askofu Mkuu Rugambwa atakumbukwa kwa kulitumikia Kanisa na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania, Vatican na mataifa mbalimbali alipokuwa akihudumu kama Balozi wa Baba Mtakatifu.

Misa hiyo imeacha ujumbe wa mshikamano, mshikamani na upendo kwa Kanisa na Taifa, huku viongozi wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza urithi wa imani na huduma uliosimamiwa na marehemu.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: