MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kujenga masoko makubwa mapya matano ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira bora zaidi.

✅ Maeneo mapya: Kinyasini, Mwera, Kibandamaiti, Kisauni na Kwahajitumbo


✅ Kupunguza msongamano na kodi kubwa kwa wafanyabiashara


✅ Kuendeleza biashara na uchumi wa Zanzibar

Rais Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara na wananchi kumchagua tena pamoja na wabunge, wawakilishi na madiwani wa CCM ili kuiongoza Zanzibar na kutimiza dhamira ya ujenzi wa masoko hayo na maendeleo kwa ujumla.

Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa wananchi kudumisha amani na kujotokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: