Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za pongezi kwa Rais mteule wa Jamhuri ya Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika, kufuatia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa Malawi wa mwaka 2025.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Rais Samia amesema pongezi hizo zinatolewa kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania, huku akisisitiza kuwa ushindi huo ni kielelezo cha imani ya wananchi wa Malawi kwa Mutharika.

“Ninawasilisha pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Profesa Arthur Peter Mutharika, Rais mteule wa Jamhuri ya Malawi, kwa ushindi katika uchaguzi mkuu wa Malawi wa mwaka 2025. Natarajia kuendelea kushirikiana naye katika kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya mataifa yetu mawili,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amempongeza Rais anayemaliza muda wake, Dkt. Lazarus Chakwera, pamoja na Chama cha Malawi Congress Party (MCP) kwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na kwa mpito wa madaraka uliojaa ustaarabu.

“Ninampongeza Mheshimiwa Dkt. Lazarus Chakwera na wananchi wa Malawi kwa uchaguzi wa amani na mchakato wa mpito ulio laini,” ameongeza Rais Samia.

Tanzania na Malawi zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu unaojikita katika historia, ujirani na ushirikiano wa kijamii, kisiasa na kiuchumi, ambapo Rais Samia amesisitiza dhamira ya kuendeleza mahusiano hayo katika kipindi kijacho.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali, Profesa Mutharika alipata zaidi ya asilimia 60 ya kura, akimshinda kwa mbali mpinzani wake Dkt. Chakwera aliyepata takribani theluthi moja ya kura. Ushindi huo unamwezesha kurejea tena madarakani miaka mitano baada ya kuondoka Ikulu ya Rais mjini Lilongwe.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: