Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Kardinali Protase Rugambwa pamoja na Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo Mhashamu Baba Askofu Paul Ruzoka mara baada ya kuwasili Ikulu Ndogo ya Tabora tarehe 12 Septemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Kardinali Protase Rugambwa pamoja na Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo Mhashamu Baba Askofu Paul Ruzoka, Ikulu Ndogo ya Tabora tarehe 12 Septemba, 2025. Pamoja na mambo mengine pia Maaskofu hao walimuombea Rais Dkt. Samia ambaye anagombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Na Mwandishi Wetu, Tabora.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), amekutana na kuzungumza na viongozi wa Kanisa Katoliki jijini Tabora.

Mazungumzo hayo yalifanyika Septemba 12, 2025, Ikulu Ndogo ya Tabora, ambapo Rais Samia alipokea maombi maalum kutoka kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Kardinali Protase Rugambwa, pamoja na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo, Mhashamu Paul Ruzoka.

Katika mazungumzo hayo, maaskofu hao walimpongeza Rais Samia kwa uongozi wake na jitihada za kuwaletea Watanzania maendeleo, huku wakimuombea afya njema, hekima na mshindi mwema katika safari yake ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Rais Samia alishukuru viongozi hao wa dini kwa maombi na ushauri wao, akisisitiza dhamira ya serikali kuendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kulinda amani, mshikamano na maendeleo ya Taifa.

Mazungumzo hayo yamekuja wakati ambapo kampeni za uchaguzi mkuu zinaendelea, huku viongozi wa dini wakihimiza amani, mshikamano na mshindano ya hoja miongoni mwa wagombea na wafuasi wao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: