Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Julai 10, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO anayeshugulikia masuala ya Utamaduni, Bw. Ernesto Ottone, pembezoni mwa Mkutano wa 47 wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendelea mjini Paris, Ufaransa.

Kupitia kikao hicho, viongozi hao wameazimia kukuza ushirikiano kati ya UNESCO na Tanzania katika uhifadhi wa Maeneo ya Urithi wa Dunia yaliyopo nchini Tanzania.
Kadhalika, Mkurugenzi huyo ameahidi kuimarisha ushirikiano katika uendelezaji wa shughuli za kiutamaduni nchini Tanzania na kukuza uhifadhi wa vivutio vyake vya kipekee.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Ali J. Mwadini, pamoja na wataalam wengine kutoka Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: