Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), imezindua rasmi nyaraka tatu muhimu za usimamizi wa maafa katika Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, tarehe 23 Julai 2025.

Nyaraka hizo ni:

✅ Mpango wa Dharura wa Wilaya (D-EPRP)
✅ Mkakati wa Kupunguza Hatari ya Maafa (D-DRRS)
✅ Ripoti ya Tathmini ya Uhitaji Baada ya Maafa (PDNA)
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Nyakia Chirukile alisema:

“Hii ni hatua muhimu kujenga mfumo wa utayari dhidi ya majanga kama mafuriko.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hosea Ndagalla, alieleza kuwa uzinduzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022.

Naye Mwakilishi wa UNDP Tanzania, Bw. Godfrey Mulisa alisisitiza umuhimu wa nyaraka hizo kwa maendeleo endelevu:

“Mpango huu ni sehemu ya kusaidia jamii kujenga upya maisha yao na kuwa imara zaidi.”

Wadau wa maendeleo walitoa pongezi kwa serikali na UNDP kwa hatua hiyo muhimu, huku wakiahidi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mipango hiyo ya kujenga uwezo wa jamii kukabiliana na maafa.

🟢 #Maafa2025 #Sumbawanga #UtayariDhidiYaMajanga #UNDP #OWM



Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: