Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (katikati) akikata utepe kuashiria kufungua rasmi duka la Vodacom lililopo eneo la kituo cha mwendokasi (SGR) cha Samia Jijini Dodoma leo. Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Vodacom Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na kushoto ni Mdau wa Vodacom, Emmanuel Makaki .
Na Mwandishi Wetu.

Dodoma – 20th Novemba 2024: Vodacom Tanzania Plc imezindua duka lake jipya (Vodashop) katika stesheni ya SGR iliyopo mkoani Dodoma huku ikiwa na mpango wa kufungua duka lingine mkoani Morogoro. Hatua hii muhimu inaonyesha dhamira ya kampuni hiyo kutoa huduma stahiki kwa wateja wake huku wakipanua wigo wa upatikanaji kote nchini. Hii ikiwa ni muendelezo wa mikakati yake ya kuhakikisha wateja wake wanapata huduma haraka pale wanapohitaji.

Ikiwa imepangwa kimkakati kuhudumia abiria wa reli ya SGR, maduka haya mapya, pamoja na la Dar es Salaam, yatakuwa vituo vinavyotoa huduma zote za kampuni hiyo. Wasafiri sasa wanaweza kupata huduma za M-Pesa, simu janja ana vifaa vyake Pamoja na msaada wa wataalam watoa huduma kwa wateja kwa urahisi, ili kuhakikisha wanaunganishwa na mtandao muda wote wa safari zao.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Vodacom Plc, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisisitiza umuhimu wa hatua hii, "tunafuraha kuzindua Vodashops hizi zilizoko ndani ya stesheni ya SGR hapa jijini Dodoma na baadae Morogoro ikiwa ni hatua muhimu katika kuwasogezea wateja wetu huduma bora. Tukitambua mchango wa SGR katika ukuaji wa uchumi wetu, tumejiandaa kutoa huduama stahiki kwa watumiaji wake. Aidha, uzinduzi huu ni sehemu ya maono yetu mapana ya kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa kidigitali kwa kuhakiisha tunawaunganisha watanzania wengi kwenye mtandao.

"Maduka haya mapya yatatoa huduma ya viwango vya juu, yakirahisisha upatikanaji wa bidhaa na huduma mbalimbali za kampuni hiyo. Upanuzi huu unaendana na maono ya Vodacom ya kukuza ujumuishwaji wa kidijitali, kuimarisha muunganisho na kusaidia ukuaji wa kijamii na kiuchumi kote nchini.
"Napenda kutoa pongezi za dhati kwa timu ya Vodacom kwa uzinduzi wa duka la Vodashop katika stesheni yetu ya SGR Dodoma. Huu ni mfano bora wa juhudi za kampuni hii katika kuboresha upatikanaji wa huduma kwa Watanzania, hasa wale wanaposafiri. Tunapongeza Vodacom kwa kuendelea kuwa mshirika katika maendeleo ya taifa ya kiuchumi. Wameendelea kuwekeza katika miundombinu ya kisasa inayosaidia kukuza uchumi na kuimarisha muunganisho wa taifa letu. Hatua hii ni muhimu katika kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma bora popote alipo”, aliongea Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule.
Uzinduzi wa SGR Vodashop unathibitisha ahadi za Vodacom za kutoa huduma bora kwa wateja wakati wote pamoja na suluhisho za kibunifu na zenye kuzingatia mahitaji ya wateja ili kuboresha maisha ya Watanzania. Wakati nchi inakumbatia mabadiliko ya kidijitali, Vodacom Tanzania inabaki kuwa taasisi yenye nguvu inayohakikisha kila mteja anaunganishwa katika mawasiliano kwa urahisi zaidi, na haswa hasa kwa wale walio safarini.

Kwa upande wake Mkuu wa Kanda ya Kati, Joseph Sayi alidokeza, "Tunatambua kuwa wateja wetu pia wanategemea sana njia za kidijitali ili kuweza kujihudumia wenyewe popote walipo,iwe ni kupitia aplikesheni ya Vodacom, M-Pesa Super App, tovuti yetu au mitandao ya kijamii, wateja wetu wanaweza kuwasiliana nasi wakati wowote, mahali popote. Tumejidhatiti kutoa huduma ndani ya maduka na mtandaoni ili kuhakikisha kuwa wateja wetu hawapati changamoto yeyote wakati wa matumizi ya huduma zetu,”.
Picha ya pamoja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: