Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa (kulia) akitoa maelezo ya awali kuhusu TPA wakati wa kikao kazi cha ofisi hiyo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu kilicholenga kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu wakati akizungumza nao kwenye kikao kazi cha kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama akitoa maelezo kuhusu ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma uliofanyika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu kuzungumza na Menejimenti ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (meza kuu) akiongoza kikao kazi na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (RPA) kilicholenga kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Timu ya Ukaguzi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi cha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu wakati akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kilicholenga kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe.Jaji (Mst) Hamisa Kalombola (kushoto) akitazama nyaraka wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakati wa kikao kazi hicho kilicholenga kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Mary Mwakapenda akifuatilia kikao kazi cha kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Stanslaus Kagisa akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) mara baada ya Naibu Waziri huyo kufunga kikao kazi na Mamlaka hiyo kilicholenga kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Na Veronica Mwafisi - Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amewataka Waajiri katika Taasisi za Umma kuwapa waajiriwa wapya mafunzo elekezi yanayostahili ili kuondokana na uvunjifu wa maadili na kushtakiana kwa sababu ya kutokuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa Umma.

Mhe. Sangu ametoa kauli hiyo wakati wa kikao kazi cha kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa Utumishi wa Umma lililofanyika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) jijini Dar es Salaam.

Mhe. Sangu amesema ni vizuri waajiri wakatafuta watu sahihi wa kutoa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya badala ya kuchukua watu wa mitaani kwani kwa kufanya hivyo kunahatarisha ajira za watumishi hao na Utumishi wa Umma kwa ujumla.

“Waajiriwa wapya wanatakiwa kuelekezwa kwa umakini wa hali ya juu ili wazijue Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma, hivyo ni vizuri wakatumika wataalam wanaoweza kufanya kazi hiyo,” Mhe. Sangu amesisitiza.

Aidha, Mhe. Sangu amesema Rasilimaliwatu ni rasilimali muhimu kuliko rasilimali nyingine hivyo ni vizuri ikasimamiwa kwa umakini ili kuleta tija kwa taifa.

“Rasilimaliwatu haitakiwi kuchezewa hata kidogo na ndio maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akiipa kipaumbele katika kuisimamia kwa kuangalia haki na masilahi ya watumishi,” Mhe. Sangu amesema.

Ameongeza kuwa mifumo mbalimbali mizuri inayoanzishwa itakuwa haifanyi kazi kikamilifu kama rasilimaliwatu itachezewa.

Amesema Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iko tayari kusimamia na kuhakikisha haki na masilahi ya watumishi wa Umma nchini yanalindwa kama ambavyo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza.

“Ofisi ya Rais-UTUMISHI itahakikisha watumishi wa umma wanatendewa haki na kulinda masilahi yao na ndio maana tumeanzisha mifumo mbalimbali ya utekelezaji wa majukumu.” Mhe. Sangu amesisitiza.

Mhe. Sangu ameipongeza Menejimenti ya TPA kwa kufanya kazi kwa kuzingatia Taratibu na Miongozo ambayo imekuwa ikitolewa na Ofisi ya Rais-UTUMISHI.

Amewataka waajiri wote nchini katika taasisi za umma kuzingatia taratibu na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kuepuka malalamiko ya watumishi na kukwamisha utekelezaji wa majukumu.

Akimkaribisha Naibu Waziri Sangu kuzungumza na Menejimenti ya TPA, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe.Jaji (Mst) Hamisa Kalombola amesema zoezi la ukaguzi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma linafanyika kwa kuzingaria sheria na sio kwa maamuzi yao binafsi.

“Ukaguzi wetu umefanyika kwa upande wa Rasilimaliwatu kwani rasilimaliwatu hiyo ndiyo inayoisaidia Serikali kutekeleza majukumu na kupanga mipango ya maendeleo hivyo ni muhimu sana kwa taasisi za umma kuzingatia hili.” Mhe. Kalombola ameongeza.

Akitoa maelezo ya awali, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa ameishukuru Tume ya Utumishi wa Umma na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuwapa ushirikiano na kutoa miongozo ambayo inawasaidia kuboresha utendaji kazi wa taasisi hiyo hasa katika eneo la usimamizi wa rasilimaliwatu.

Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma ni njia mojawapo ambayo hutumika kupima ni kwa kiwango gani, Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu wanazingatia Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma katika kusimamia Utumishi wa Umma.

Tume ya Utumishi wa Umma chini ya Kifungu cha 10(1(c) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298, imepewa mamlaka ya kufuatilia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu katika usimamizi wa Utumishi wa Umma ikiwemo usimamizi wa masuala ya Rasilimali Watu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: