Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka akitoa mada katika semina hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Patrick Kipangula akifafanua jambo katika semina hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu kwa Mpiga Kura Bi. Giveness Aswile akifafanua jambo katika semina hiyo.

Na Mwandishi Wetu.

Serikali imewataka wanahabari nchini kutambua kuwa wana nafasi kubwa ya kuelimisha jamii ili kuweza kushiriki kikamilifu katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini.

Hayo yamesemwa leo Juni 14 jijini Dar es Salaam na Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka wakati wa semina ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini iliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Vyombo vya habari vina ushawishi mkubwa katika jamii ukiona jamii ya sasa wamachozungumza na wanachojadiliana asilimia kubwa kintokana na ushawishi wake vyombo vya habari,” amesema Mhandisi Kisaka.

Amesema kuelimisha wananchi lazima kuwe na, weledi, maadili katika taaluma vizingatiwe ili kuhakikisha umma unajisikia faraja kushiriki katika maboresho hayo bila kusita.

Pia amesema wanaunganisha jamii katika masuala ya kitaifa na kuchochea maendeleo katika jamii.

“Nawataka Wanahabari kutambua kuwa wao ni watoa huduma katika jamii na huduma inayotolewa inatambulika kuwa ni haki ya msingi kiraia na haki ya kila mtu,”amesema

Ameeleza kuwa sera ya habari na Utangazaji ya mwaka 2003 inatambua sekta hiyo kuwa ni sekta ya huduma za jamii nchini kwa kutoa na kupokea habari inatambulika duniani kote kuwa ni moja ya haki za msingi.

“Idadi ya watu wanaofikiwa na utangazaji wa televisheni kwa njia ya setelite (DTH) ni asilimia 100 Idadi watu wanafikiwa na utangazaji na televisheni kutumia miundombinu ardhini (DTI) ni asilimia 56 na Idadi ya visambuzi ni milioni 3.8,”amesema.

Mhandisi Kisaka amesema hadi kufikia machi 2024 Idadi ya watumiaji wa simu janja imeongezeka kufikia asilimia 32.59.kutoka asilimia 32.13 iliyorekodiwa Disemba 2023.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Patrick Kipangula amesema wanahabari wanapaswa kutoa habari za kweli na kwa usahihi kwa umma wakati wote wa uchaguzi ili kuwajengea amani na utayari wananchi waweze kuboresha taarifa zao

“Kupotosha taarifa zisizo sahihi kunaweza kusababisha hofu, kuchochea, ghasia kupunguza imani ya wananchi kwenye mchakato wa uchaguzi, “amesema Kipangula.

Amesema kanuni na usawa na haki kutoa nafasi sawa kwa wagombea wote na vyama vyote vya siasa pia kufuata kanuni, sheria na maadili ya habari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mtibora Seleman amesema wataendele kushirikiana na wanahabari katika kusukuma maendelo ya Taifa katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Aidha amesema Tume itaendelea kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwasababu wanapata haki zao msingi za kikatiba.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: