Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV.

MJUMBE wa Baraza Kuu UWT Taifa ambae pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi Wanawake Mkoa wa Pwani Mariam Ulega amechangia Sh. milioni 3 kwa kikundi cha Pwani Generation Queens (Mwanamke Sahihi Fete) ili kuunga mkono kampeni ya kumsaidia baiskeli mtoto mwenye ulemavu wa viungo.

Akizungumza katika hafla ya kutimiza miaka saba ya kikundi hicho iliyoambatana na utoaji tuzo ya Kazi IENDELEEE AWARDS kwa makundi mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, Mariam Ulega amewapongeza kwa jitihada zao za mkomboa mwanamke na kusaidia makundi yenye mahitaji.
"Niwapongeze Kwa kuanzisha harambee ya kumkomboa mtoto mwenye ulemavu wa viungo kwani ni suala muhimu. Pia nawapongeza kwa kuandaa tuzo za kazi Iendeleee ,kwani itakwenda kutoa hamasa watu kujituma na mimi nawashukuru kwa kunipatia Tuzo ya Heshima kwa hakika mmeniheshimisha," amesema.
Aidha amewahakikishia watakuwa pamoja kuhakikisha mwanamke wa Mkoa wa Pwani anasonga mbele kwa kasi ya 5G na kwamba Umoja wao ndio ushindi wao,hivyo wafanye kazi na kuendelea kusaidia wenye mahitaji maalum.

Amewataka wanawake kuiga kwa vitendo yale mazuri yanayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kusisitiza wanayo kila sababu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais katika kuleta maendeleo ya Watanzania wote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha Pwani Generation Queens (MWANAMKE SAHIHI FETE) mkoani Pwani, Betty Msimbe amesema hii ni mara ya tatu wamekuwa wakitoa tuzo hiyo na kusisitiza itaakuwa endelevu kwani ni jambo jema.

Kuhusu tuzo hizo amesema wanatoa kama sehemu ya kutambua jitihada za watu mbalimbali ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kuleta maendeleo.

Pia amesema wameanzisha kampeni ya KOMBOA WATOTO WENYE ULEMAVU ambapo lengo lao kupata baiskeli 100 lakini hadi sasa wameshatoa 26.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: