Na Mwandishi Wetu
Diwani wa Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo mkoani Dar es Salam, Bakari Kimwanga, amewataka wanawake na vijana kuchangamkia fursa za mikopo zinatolewa na Benki ya CRDB
Hayo ameyasema leo alipokuwa akifungua mafunzo ya wajasiriamali wa Kata ya Makurumla yaliyoendeshwa na ofisi yake kwa kushirikiana na Benki ya CRDB.
Amesema suala la fursa ni muhimu jambo ambalo aliliahidi katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumzo katika mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na wajasiriamali zaidi ya 400 wa kata hiyo, amesema kuwa ni lazima jamii ikubali kubadili mwenendo kwa kuhakikisha kila anayekopa mkopo anafanyia shughuli za uzalishali ambayo itakuwa na manufaa kwa familia na Taifa kwa ujumla.
"Ndugu zangu mwaka 2020 sie tuliyasema mengi kwenu ikiwamo kuzitafuta fursa hasa za mafunzo na mikopo kupitia taasisi mbalimbali. Ninawashukuru Benki ya CRDB na leo wamekuwa na watalaamu wao wa kutosha hapa watatoa mafunzo ya utengenezaji wa batiki, sabuni na kisha mfungue akaunti ikiwamo wa Malkia ili muweze kujiwekea akiba.
"Ninajua leo kila mmoja atataka hapa kusikia kuhusu mikopo, ndio ni haki yenu kubwa ninawaomba muende mkope mikopo kwa ajili ya kununua malighafi na vifungashio vya bidhaa zenu za kisasa ili ziweze kupata soko la ndani na nje ya Tanzania.
"Katika jamii yetu ya wana Makurumla tukifanikiwa kutoa mafunzo haya kwa wanawake na vijana ni wazi tutakuwa tumeikomboa jamii yetu katika vita dhidi ya umaskini na sasa tuchangamkie fursa hii,"amesema Kimwanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: