Kaimu Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Opra Msuya kulia akisisitiza jambo kwa Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati walipowatembelea wakati wakiadhimisha sherehe za shukrani ambapo walitembelea wodi ya watoto kwenye Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kugawa misaada mbalimbali ikiwemo kuhaidi kutoa fedha za matibabu za wagonjwa wawili kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia akimkabidhi mmoja msaada ya vitu mbalimbali Kaimu Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Opra Msuya

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizngumza mara baada ya kukabidhi msaada huo


Na Oscar Assenga,TANGA.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga imeadhimisha sherehe za shukrani kwa kuwatembelea wodi ya watoto kwenye Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kugawa misaada mbalimbali ikiwemo kuhaidi kutoa fedha za matibabu za wagonjwa wawili kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Ugawaji wa msaada huo wenye thamani ya Milioni 3.5 ulitolewa katika wodi ya watoto katika halfa iliongozwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akiwa ameambatana na maafisa mbalimbali wa mamlaka hiyo na watumishi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa uongozi wa Hospitali hiyo Meneja Specioza alisema kwamba wao katika kuadhimisha wiki ya shukrani kwa mteja waliona watoe shukrani kwa walipa kodi wao kwa kuwapatia msaada huo.

Alisema kwamba walishakutana na wafanyabiashara wao na kwamba katika kipindi hiki wamekuwa na utaratibu wa kuwambuka jamii inayowazunguka hivyo wameona kutembelea hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kutembelea wodi ya watoto.

Meneja huyo alisema kwamba wametoa shukrani kwa jamii kutokana na kwamba wamaani jamii ikiwa imara na afya bora na kodi itaongezeka maana wanapokuwa na afya ndipo wana pata nguvu za kufanya biashara na kulipa kodi stahiki.

“Tumeona tuje tuwaone watoto tujue matatizo yao na tunalengo la kuwakatia bima ya afya watoto 25 kwa sababu kuna watoto wengi wanahitaji bima lakini wakati tunaendelea na watoto wao tumetembelea pia wodi ya watu wazima tukakutana na wagonjwa wawili.

Alieleza kwamba wagonjwa hao walikuwa wanahitaji msaada wa kufanyiwa upasuaji ambao ni Frank na Mzee Hamisi na hivyo watatoa fedha kuwasaidia waweze kuwafanyiwa upasuaji ikiwa ni kusheherekea sherehe ya kuwashukuru walipa kodi na jamii kwa ujumla.

Awali akizungumza wakati akipokea msaada huo. Kaimu Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Opra Msuya aliwashukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga kwa kuwapatia msaada huo wagonjwa hasa kwa ajili ya wenzao wenye uhitaji mungu awabariki wanawaomba wasiiishie hapo waendelee kujitolea.

Hata hivyo kwa upande wake mmoja wa wagonjwa ambaye alipatiwa msaada wa kufanyiwa upasuaji Frank Beda anayetokoea wilayani Muheza aliyegongwa na aliyehusika na tukio hilo alikimbia aliwashukuru TRA kwa kuwapatia msaada huo na kwamba mwenyezi mungu awabariki sana katika maisha yao
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: