Kapteni Abdallah Hussein Nyige akimpima mapigo ya moyo Private Sunday Makobwe kulia ni Naibu Waziri akishuhudia.
Afisa wa JWTZ akimpima uzito Mwananchi kwenye zoezi hilo.
Mgeni rasmi Mhandisi Kundo Mathew akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka JWTZ.
Naibu Waziri akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari.
Na Khadija Kalili, Kibaha
NAIBU Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano Mhandisi Kundo Mathew ametoa wito kwa wakaazi wa Wilaya ya Kibaha kujijengea utamaduni wa kuangalia afya zao kwa kufanya vipimo mbalimbali jambo ambalo litastawisha afya ya jamii.
Mhandisi Kundo amesema hayo leo Agosti 16 alipokuwa mgeni rasmi kwenye zoezi la upimaji afya kwa wananchi wa Kibaha lililohusisha wanawake na watoto , lilioandaliwa Taasisi inayotetea haki ya Mama na Mtoto TAWOJAC, Taasisi ambayo inaundwa na Waandishi wa Habari Wanawake.
Naibu Waziri huyo amtoa pongezi zake za dhati kwa TAWOJAC kwa namna walivyojitoa kwa kuwakumbuka wananchi hasa kwenye suala kubwa na lenye umuhimu la afya ya mama na mtoto.
Mkurugenzi wa TAWOJAC Neena nchimbi amesema TAWOJAC imejikita kupima Afya ya Mama na Mtoto bure ili kuisaidia serikali kwa upande wa afya na kuwa wameanzia Mkoa wa Pwani ambapo wameshirikiana na wataalamu wa afya kutoka Jeshi la wananchi JWTZ .
Kapteni Abdallah Hassan Nyige alisema mbele ya Naibu Waziri kuwa wamefurahishwa na muitikio wa wananchi wa Kibaha huku akisema kuwa katika upimaji huo wamegundua kua kuna watu huwa wanatembea huku mapigo yao ya moyo yakiwa juu isivyokawaida na huenda ikapelekea kupata madhara bila kujua ,jambo ambalo ni muhimu kila mtu akajenga utamaduni wa kupima magigo yake ya moyo mara kwa mara.
Mkuu wa Kikundi Cha Upimanji Cha JWTZ Luteni Kanali Tumenye Mwalukunga alisema kuwa wataalamu hao wamekuwa walifanya mazoezi hayo ya upimaji wa afya mara kwa mara huku akisema kuwa lengo kuu la zoezi hilo ni kuwapima kina mama saratani la shingo ya mlango wa kizazi pamoja na saratani ya matiti huku wale ambao wamegundulika kuwa na viashiria wamepewa Rufaa ya kwenda katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: