Inafahamika kuwa waha au kabila la Ha ni moja ya kabila kutoka Wabantu wa wshariki. Wabantu hawa walipata kufika maeneo hayo hata kabla ya miaka ya 600. Na ifahamike kuwa asilimia kubwa ya makabila mengi yaliyopo hapa Afrika yalipata majina kulingana na wageni walivyoelewa au walivyoona. Na kuna makabila yalipata majina kutokana na namna wanavyopigana, yapo makabila yaliopata majina namna wanavyopiga makelele na wangine walipewa majina kulinga na lugha yao au matamshi yao.
Kwa upande wa kabila la Waha ambao wengi tunafahamu kuwa wanapatikana katika mkoa wa Kigoma. Ukweli ni kwamba kabila hili ni miongoni mwa kabila ambalo lina historia kubwa sana tangu walipofika katika ardhi hiyo. Kwa mujibu wa Chubwa na masimulizi kutoka kwa baadhi ya wakazi wa Kigoma na wanahistoria wanakubaliana kuwa.
Kipindi watu hawa wanafika maeneo ya Afrika mashariki hawakujikana kama kabila la Ha na hawakuja wakiwa na kundi moja. Bali walikuja kwa mtindo wa Koo au ukoo. Na kila ukoo(ipo makala kwa ajili ya koo zao) ulikuwa na jina lake.
Ukoo au koo zilipokuwa hapo zilipata kumiliki ardhi. Na cha msingi ni kwamba watu hao walifanikiwa kuta majina ya maeneo waliyokaa kutoka na mazingira yake. Kwa mfano kuna ukoo uliokaa sehemu zenye udongo(Bayungu) walijiita Wayungu na wale waliokaa sehemu za mwinuko(Heru) walijiita Wanyaheru. Lakini mpaka kufikia miaka ya 1800, koo hizo ziliungana na kuishi sehemu na kutawaliwa na chifu mmoja. Na hapo ndipo watu hao walianza kupata jina moja lililowatambulisha kwa wageni. Sasa kwa nini watu hao waliitwa Waha. Hii ndiyo mitazamo iliyosimulia asili ya neno Waha au Ha.
1. Wapo waliodai kuwa asili ya neno Waha au Ha ni pale wageni walipofika katika ardhi ya Kigoma na kuwauliza watu hao kuwa “ ninyi ni wakina nani” na ndipo watu hao walipojibu “tur; Abhaha” wakimaanisha “ sisi ni wazaliwa wa hapa hapa. Na hapo wageni hao walikalili kuwa Waha kwa kuchukua neno “ha”
2. Wapo wanaodai kuwa wageni walipokuja na kukuta ufalme wa Buha umekuwa na ulikuwa na watu wengi, walimuuliza mfalme wao kuwa “hawa ni wakina nani” na ndio mfalme wa Buha alipojibu kuwa “N’abhaha” akimaanisha kuwa “ hawa ni wenyeji wa hapa hapa” na hapo wageni hao walipata neno “Ha” na walipoandika waliaandika hivyo.
Maelezo haya yalitolewa kwa mujibu wa watu walikuwa wamekutwa katika ardhi ya Buha. Kwa upande mwingine, historia inafafanua kuwa, Watusi walikuwa watawala wa kabila la Waha. Na kuna mahususiano makubwa sana katika ya Watusi na Waha. Na hivyo hata neno Waha bado lilionekana kuhusiana na Watusi.
Kwa Watusi neno Abaha lina maana ya mtu yeyote “anaowapa ardhi” na kwa Watusi aliyekuwa akitoa ardhi alifahamika kwa jina la Mtoke. Na mteko alikuwa akitoa ardhi kwa Watusi, walifahamika kwa jina moja la Uwaha. Na waliolima shamba moja na Mteko walijiita “Abhaha” na hata kuna baadhi ya Watusi hujiita “ Waha” na ndio maana hata walivyotawala walijiita hivyo na wageni walijua habari hizo. Na hii ndio historia fupi ya asili ya neno Waha. Na kwa nini mkoa wao uliitwa Kigoma, hiyo ni historia nyingine….
Waha ni wahutu wa kiburundi walokimbia njaa kwao nakuhamia ndani ya ardhi ya tanganyika.Kilugha chao kihaa na kirundi hamna tofauti wanalewana lugha majina yao pia yamefanana hamna tofauti.
ReplyDeleteAcha ujinga we mchangia mada
DeleteHistoria inasema kigoma haikuwa sehemu ya Tanganyika sasa unavyosema waha ndio walikimbilia Tanganyika unafahamu historia kabla ya kuongea uliza uelimishwe
DeleteNice
ReplyDeletenaomba mnisaidie maana ya jina Nsoholo
ReplyDeleteWabembe wameingia katika ardhi ya kigoma mwaka 1200 waha wamewakuta hapa wabembe na waliomzika Livingstone wale watatu walikuwa hao , kilichozikwa ni utumbu mwili ulipelekwa ulaya... Hata ukiangalia majina ya miji ao vijiji vingi ni majina ya kibembe kama ilala ngulu, kibondo(yaani Mmbondo ) ndo jina halisi la Mmbembe... Kihinga, kuna wilaya ya uvinza ( wavinza ) kihistoria ya babu zetu ndo watani wawabembe kwa miaka 600 iliopita,
ReplyDeletewabembe hawakutangulia waha bali wabembe ni wageni wajanja ukitaka kujua hilo popote mbembe alipo nje ya mkoa hujiita muha na hupenda kuwa juu ya wenyeji kama unabisha naomba uniambie machief wa kibembe hata watatu nitakukubalia ila pongezi kwa wabembe mf mzee Majuto alikuwa muwazi kuhusu kuwa mbembe lakin Tanga kuna waha walijificha elewa
DeleteWabembe wameingia katika ardhi ya kigoma mwaka 1200 waha wamewakuta hapa wabembe na waliomzika Livingstone wale watatu walikuwa hao , kilichozikwa ni utumbu mwili ulipelekwa ulaya... Hata ukiangalia majina ya miji ao vijiji vingi ni majina ya kibembe kama ilala ngulu, kibondo(yaani Mmbondo ) ndo jina halisi la Mmbembe... Kihinga, kuna wilaya ya uvinza ( wavinza ) kihistoria ya babu zetu ndo watani wawabembe kwa miaka 600 iliopita,
ReplyDeleteKigoma nakupenda sana mkoa wangu wilaya YANGU uvinza
ReplyDeleteKiongozi wa Waha anajulikana kwa jina gani?
ReplyDelete