Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa taarifa juu ya watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya matibabu bure. (Picha na Mpiga Picha Wetu)
Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa taarifa juu ya watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya matibabu bure.( Picha na Mpiga Picha Wetu)
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Tawi la Zanzibar, Ismail Kangeta, akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya matibabu itakayoanza kutolewa bure kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. (Picha na Mpiga Picha Wetu)
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kutoa muda wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo, Zanzibar.(Picha na Mpiga Picha Wetu)
Mwananchi wa Jimbo la Kikwajuni akisoma kipeperushi kilichotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambacho kina majina ya Hospitali ambazo wafaidika wa huduma ya matibabu bure wanaweza kwenda kupata huduma hiyo wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo Kikwajuni Zanzibar. (Picha na Mpiga Picha Wetu)
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Salim Jazeera (kulia), akimsikiliza mwananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kutoa muda wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo, Zanzibar.(Picha na Mpiga Picha Wetu)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: