Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo kwa baadhi ya makamanda wa Polisi wa mikoa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Agosti 12, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Pili Omary Mande aliyekuwa Afisa Mnadhimu namba moja mkoa wa Ruvuma anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi.

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marco Chillya ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi amehamishiwa mkoa wa Ruvuma akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joseph Konyo ambaye amestaafu.

Aidha aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gaudianus Kamugisha amehamishiwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Uguja, akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa wa Polisi (ACP) Abdallah Haji Seti aliyehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: