Waziri wa madini ya Tanzanite Dotto Biteko akionyesha vipande viwili vya madini ya Tanzanite
Na Pamela Mollel, Mererani

Serikali imemtangaza Bilionea mpya wa madini ya Tanzanite Anselem Kawishe kupata vipande viwili vya madini hayo venye thamani ya bilioni 2.25

Katibu mkuu wizara ya madini Adolf Nduguru alimtangaza bilionea huyo leo( 27/8/2022)katika mji mdogo wa mererani katika hafla ya ununuzi wa madini

Alisema kuwa Bilionea huyo anaandika historia nyingine kwa kupata madini yenye uzito wa kilogram 5.22

"Uwepo wa upatikanaji wa madini haya utasaidia kuitangaza Tanzania kimataifa pamoja na sekta ya madini kwa ujumla "alisema Nduguru

Aliongeza kuwa Wizara hiyo kwa mwaka 2022/23 imejipanga kukusanya mapato zaidi ya Bilioni 82

Kwa upande wake Waziri wa madini Dotto Biteko alisema kuwa ununuzi wa madini hayo umeshirikisha pande zote mbili na kufikia uamuzi wa kuuzia serikali

Waziri Biteko aliwataka wamiliki wa migodi pamoja na wachimbaji kufanya kazi kwa uaminifu kwa maslahi Taifa

"Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan iko katika mpango wa kujenga kituo cha Tanzanite City Mkoani Manyara kwa lengo la kuborsha eneo hilo pamoja na serikali kujipatia mapato"alisema Biteko

Kwa upande wake Bilionea mpya kawishe alisema amepata madini hayo baada ya kusota kwa miaka 15

"Namshkuru Mungu serikali pamoja na familia yangu nimefurahi kuona serikali inanunua madini haya"alisema Kawishe.
Gavana wa Benki kuu, Profesa Florence Luoga akionyesha vipande viwili vya madini ya Tanzanite
Kamishna wa sera wizara ya fedha na mipango Elijah Mwandumbya akionyesha vipande viwili vya madini ya Tanzanite
Bilionea mpya wa madini ya Tanzanite Anselem Kawishe akionyesha vipande viwili vya madini ya Tanzanite yenye thamani ya bilioni 2.25
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: