Serikali imezindua mwongozo wa namna ya kutumia makundi ya nyuki kwenye huduma za uchavushaji wa mimea na mazao shambani utakaowasaidia wakulima na wafugaji nyuki nchini kupata manufaa zaidi kuliko kupata asali tu.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mwongozo huo, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda anasema mwongozo huo utasaidia wafugaji na wakulima kubadirika na kumuona mdudu nyuki kuwa ana thamani kubwa na kufanya kila linalowezekana kuweza kumtumia vizuri ili kujiongezea kipato.

Kwa kuonesha ukweli kwamba uchavushaji ni kipato, Pinda anatoa mfano wa faida inayopatikana kwa mkulima na mfugaji nyuki anayekodisha makundi yake ya nyuki kwa mkulima mwingine.

Amasema mfugaji nyuki anaweza kuwakodisha wakulima wengine mizinga ya nyuki kwa kipindi cha msimu mmoja wa zao ambapo uzalishaji wa zao husika utaongezeka na mfugaji nyuki akilipwa ada ya uchavushaji huku pia uzalishaji wake wa mazao ya nyuki ukiongezeka maradufu.

“Ziko nchi nyingine kwa kutambua kuwa nyuki ni wachavushaji wakuu wanaotoa uhakika wa chakula wameiweka sekta hii chini ya Wizara ya Kilimo, tubadirike tukifanya vizuri kwenye ufugaji nyuki tutakuwa na uhakikia wa chakula lakini pia nchi nyingi tutazishinda kwa uzalishaji asali.

“Sisi hapa tunauwezo wa kuzalisha hadi tani 140,000 na kuendelea kwa utajiri tulionao tatizo tu ni kwamba hatujafunguka licha ya Serikali kuonyesha dhamira ya wazi ya kutaka kukuza sekta ya ufugaji nyuki,” anasema Pinda.

Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Mkurugenzi wa misitu na nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii nchini anasema mwongozo huo ni mkakati wa kuwasaidia wafugaji nyuki kuanzia kwenye uandaaji wa makundi ya nyuki, utunzaji wake wakiwa shambani hadi namna ya kuingia makubaliano.

Miongoni mwa vipengere ambavyo mwongozo huo unaelezea ni namna ya kuandaa makundi ya nyuki kwa ajili ya uchavushaji, usimamizi wa makundi hayo ya nyuki yakiwa shambani, utaratibu wa kuyarudisha makundi ya nyuki baada ya uchavushaji mahali unapoyatunza, usalama na huduma ya kwanza katika shamba linalopata huduma ya uchavushaji na masula ya kuzingatia wakati wa kupanga bei ya ukodishaji makundi ya nyuki.

“Wadau wanapaswa kuuelewa mwongozo huu, na ni lazima kuufuata lakini huu ni mwongozo wa kwanza kutolewa hivyo tunaimani unaweza ukawa na mapungufu, hivyo basi tunakaribisha maoni ya wadau kwa jinsi watakavyokuwa wakiutumia,” alisema.

Mkurugenzi Mwakalukwa amesema mwongozo huo umezinduliwa baada ya tafiti kuonyesha kulikuwepo na uendeshwaji wa bishara ya kukodisha makundi ya nyuki pasipo kuwa na utaratibu.

Baadhi ya wafugaji nyuki wamesema, mwongozo huo umekuja wakati muafaka na unaonyesha wazi dhamira ya Serikali katika kuwakomboa kiuchumi wafugaji nyuki nchini. Tulizo Kilaga anaripoti.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: