MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo kushoto amkizungumza na waandishi wa habari kuhusu mapato yaliyokusanywa na Jiji hilo ikiweno kufafanua taarifa iliyotangazwa kutoka kwa Waziri wa Tamisemi Inocent Bashungwa kuhusu Jiji hilo kuongoza kwa ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022.
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo amesema Jiji hilo linatarajia kuboresha vyanzo vya mapato ili viweze kuongeza ukusanyaji vizuri, kuvisimamia vema ili kuweza kuepuka mianya ya upotevu wa fedha za Halamshauri.
Shilloo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mapato yaliyokusanywa na Jiji hilo ikiweno kufafanua taarifa iliyotangazwa kutoka kwa Waziri wa Tamisemi Inocent Bashungwa kuhusu Jiji hilo kuongoza kwa ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022.
Alisema kwamba wanaboresha vyanzo hivyo kwa mapato ambapo kwa kuliona hilo bajeti yao 2021/2022 ilikuwa ni bili 15.354 lakini bajeti yao wanayoiomba ipitishwe ya 2022/2023 ni bilioni 16 iliongozwa asilimia 4 na wanakwenda mbele na hawashuki nchini maana yake ni kukusanya fedha zaidi.
Mstahiki Meya huyo alisema ni matarajio ya baraza la madiwani lilionigia mwaka juzi ndani ya miaka mitano wafikishe bilioni 20 na ndio thamira yao kwamba watoke kwenye bilioni 15 mpaka Bilioni 20 wastani ya kila mwaka kuongeza Bilioni 1.
Alisema pili Halmashauri wanafikiria kuongeza vyanzo vyengine vya mapato mojawapo ikiwemo ujenzi wa jengo la Kitega uchumi lililopo eneo la Kange Stendi na wanategemea litaongeza mapato.
Aidha alisema pia wana mpango muda mrefu ndani ya miaka mitano kujenga machinjio ya kisasa Pongwe kutokana na kwamba yaliyopo kwa sasa ya Sahare yamepita na wakati na ya muda mrefu na hayana taswira ya Jiji hilo.
“Machinjio haya yatatoa huduma bora kwa jamii ya watu wa Tanga na kuchochoea uchumi na kutoa huduma bora kwa jamii na tumejipanga kuanzisha soko kubwa la kisasa Pongwe litakuwa linauza mazao ya jumla “Alisema
Alisema maana yake wanahitaji magari makubwa yanayoleta bidhaa kutoka nje ya Jiji la Tanga yaishie Pongwe ili nayo liweza kupeleka kwenye masoko mengine yaliyopo Tanga ni moja ya kitega uchumi.
Hata hivyo alisema pia wanakusudia kuimarisha masoko yaliyopo moja Mgandini kuwa la kisasa na kuiamrisha na kukarabati soko la Mlango wa Chuma, Makorora, Ngamiani na mengine yataimarishwa ili yaweze kuwa ya kisasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: