Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pili kulia) na, Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Gilitu Makula (katikati) wakikabidhi nondo kwa Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya na Mkuu wa Gereza la wilaya ya Shinyanga sehemu ya Gereza la Wanawake ASP Grace Thomas Massawe (kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amepokea na kukabidhi vifaa vya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’ vilivyotolewa na wadau mbalimbali ili kukabiliana na uhaba wa malazi unaotokana na changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu.

Vifaa hivyo vya ujenzi wa bweni katika gereza la wilaya ya Shinyanga vinatokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Shinyanga ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Jasinta Mboneko katika kuondoa changamoto zilizopo kwenye gereza hilo ambalo limeelemewa na idadi ya wafungwa na mahabusu.

Akizungumza leo Jumanne Februari 1,2022,wakati wa kupokea na kukabidhi vifaa vya ujenzi wa bweni la Magereza, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amewashukuru wadau waliojitokeza kuchangia ujenzi huo na kuwaomba wadau kuendelea kujitokeza kuchangia ujenzi wa bweni hilo.

“Kuna msongamano mkubwa wa wafungwa na mahabusu katika gereza hili. Kutokana na changamoto hii tuliwaomba wadau watushike mkono katika ujenzi wa bweni jipya. Tunawashukuru sana wadau mliojitokeza kuchangia ujenzi huu. Tuliwaita na mkaitikia mara moja na tunawaomba wadau wengine wajitokeze, hata kama una matofali 10 wewe tuletee tunayapokea, na sasa kazi ya ujenzi inaanza mara moja”,amesema Mboneko.

Ameeleza kuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi, bweni hilo jipya litakuwa na uwezo wa kubeba wafungwa na mahabusu 100 na kwamba wanaendelea na jitihada za kutafuta magodoro kutoka kwa wadau wakiwemo GSM kwa ajili ya wafungwa na mahabusu.

Mboneko amewataja miongoni mwa wadau waliojitokeza kutoa michango ya ujenzi wa Bweni katika gereza la Shinyanga ni Kampuni ya Aham Investment Co. Ltd ambayo imechangia matofali 1,000,TANROADS Mkoa wa Shinyanga tripu tano za mchanga na Kampuni ya Jonta Investment Co. Ltd mifuko 100 ya saruji.

Wadau wengine waliokabidhi vifaa vya ujenzi leo ni Kampuni ya Gilitu Interprises Ltd ambayo imechangia shilingi Milioni moja kwa ajili ya nondo na yeye mwenyewe (Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko) akichangia shilingi Milioni moja kwa ajili ya ununuzi wa nondo na wamekabidhi nondo 88.

Wakikabidhi vifaa hivyo wadau hao akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Aham, Ally Ameir, Amina Mikuki kutoka Kampuni ya Jonta Investment Co. Ltd, Mhandisi Mwandamizi kutoka TANROADS Joseph Mayaya na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Gilitu Makula wameishukuru serikali kuona umuhimu wa kushirikisha wadau katika ujenzi huo wa bweni la magereza kwani serikali pekee haiwezi kumaliza changamoto zilizopo katika jamii.

Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya amewashukuru wadau kwa mchaango wa vifaa vya ujenzi na kwamba mara baada ya kupokea vifaa vya ujenzi shughuli ya ujenzi inaanza mara moja na wanategemea kukamilisha ujenzi huo ndani ya wiki mbili kwani mafundi wamo humo humo gerezani.

Ameeleza kuwa gereza hilo lina uwezo wa kubeba wafungwa na mahabusu wa kiume 130 na wa kike 30 (jumla 160) lakini idadi imekuwa ikipanda hadi kufikia zaidi ya 450 hiyo kusababisha changamoto kubwa ya malazi huku akiomba wadau kuwapatia magodoro kwani yaliyopo ni machache.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza leo Jumanne Februari 1,2022 wakati akipokea na kukabidhi vifaa vya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’ vilivyotolewa na wadau ili kukabiliana na uhaba wa malazi unaotokana na changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’ vilivyotolewa na wadau ili kukabiliana na uhaba wa malazi unaotokana na changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akiangalia matofali 1000 yaliyotolewa na Kampuni ya Aham Investment Co. Ltd wakati akipokea na kukabidhi vifaa vya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akipokea matofali 1000 kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Aham Investment Co. Ltd, Ally Ameir kwa ajili ya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akipokea mifuko100 ya saruji kutoka kwa wawakilishi wa Kampuni ya Jonta Investment Co. Ltd, Amina Mikuki na Mchungaji Japhet Kilago (kulia) kwa ajili ya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akiwashukuru wawakilishi wa Kampuni ya Jonta Investment CO. Ltd, Amina Mikuki na Mchungaji Japhet Kilago (kulia) kwa kuchangia mifuko100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiangalia sehemu ya tripu za mchanga uliotolewa na TANROADS mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pili kulia) na, Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Gilitu Makula (katikati) wakikabidhi nondo kwa Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya na Mkuu wa Gereza la wilaya ya Shinyanga sehemu ya Gereza la Wanawake ASP Grace Thomas Massawe (kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’.
Amina Mikuki kutoka Kampuni ya Jonta Investment Co. Ltd (kulia) akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi wa Bweni katika Gereza la Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Aham, Ally Ameir (kulia) akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi wa Bweni katika Gereza la Shinyanga.
Mhandisi Mwandamizi kutoka TANROADS Shinyanga Joseph Mayaya ( wa pili kushoto) akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi wa Bweni katika Gereza la Shinyanga.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi (kushoto) akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi wa Bweni katika Gereza la Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Gilitu Makula akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi wa Bweni katika Gereza la Shinyanga.
Mkuu wa Gereza la wilaya ya Shinyanga sehemu ya Gereza la Wanawake ASP Grace Thomas Massawe (kulia) akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi wa Bweni katika Gereza la Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na maafisa wa gereza la Shinyanga na wadau baada ya kupokea na kukabidhi vifaa vya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’ vilivyotolewa na wadau ili kukabiliana na uhaba wa malazi unaotokana na changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu.
Muonekano wa sehemu ya vifaa vya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’ vilivyotolewa na wadau ili kukabiliana na uhaba wa malazi unaotokana na changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu.
Muonekano wa sehemu ya vifaa vya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’ vilivyotolewa na wadau ili kukabiliana na uhaba wa malazi unaotokana na changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu.
Muonekano wa sehemu ya vifaa vya ujenzi wa bweni ‘sero’ mpya katika gereza la wilaya ya Shinyanga maarufu ‘Mhumbu’ vilivyotolewa na wadau ili kukabiliana na uhaba wa malazi unaotokana na changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: