MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka
Na Mwandishi Wetu Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amegoma kupitisha kibali cha bajeti ya shilingi Milion 47 iliyoombwa na madiwani wa Jiji na watumishi kwa ajili ya ziara ya kwenda Jijini Mbeya kujifunza usafi wa mazingira,ukusanyaji wa mapato,kutokomeza ziro,shule za michepue ya kiingereza na utekelezaji wa sheria ndogo na kamati zake.
Sambamba na hilo Mkuu huyo amesema fedha hizo haziwezi kupitishwa kwa sababu Jiji la Dodoma bado lina changamoto nyingi.
Akizungumza leo kwenye kikao na watumishi wa Jiji la Dodoma,Rc Mtaka amesema ikumbukwe kwamba hakuna kiongoziara yoyote wa serikali kutokomeza nje ya Mkoa wake Mpaka pale miradi ya kimaendeleo itakapokamilika au uwe na oda maalum kutoka ngazi za juu.
"Naomba nitoe Maelekezo kama Mkuu wa Mkoa na kwa Jiji kwa ujumla viongozi wajitafakari kamati kuna haja ya kutumia Milion 47 kwa ajili ya kujifunza usafi wa mazingira na mambo mengine wakati huyo tunakotaka kwenda kujifunza kuna changamoto nyingi kuliko Mkoa wetu wa Dodoma,"
Ameongeza kusema Mkoa wa Dodoma una miradi mingi na mikubwa kwanini madiwani watake kwenda Jijini mbeya kwenda kujifunza utekelezaji wa sheria ndogo na kamati zake wakati kuna nafasi ya kuteua kamati ndogo kwenda kujifunza sheria hizo.
Kwa upande mwingine amewataka watumishi wa Jiji waache kutumia kutoa lugha za ovyo na majibu mabaya pindi wanapohudumia wananchi.
"Mbaya zaidi ubaya wenu mmekuwa mkifanyiana hata wenyewe kwa wenyewe kwa kuwekeana fitina majungu na uchonganishi hali inayopelekea kuleta shida kwa wananchi tunaowahudumia"amesema Mtaka
"Kama unaona kero kupigiwa simu nenda kafanye kazi kwa wahindi lakini kama mtumishi wa umma lazima usikilize kero za watu wote wajinga,werevu,na wajuaji na ikitokea umeshindwa kuwasikiliza watu hao kazi ya utumishi wa umma itakushinda"ameongeza Mkuu wa Mkoa
Kwa upande mwingine amewataka viongozi wa Jiji akiwemo mkurugenzi na timu yake wakae na kumaliza matatizo ya wananchi kwani katika Jijini hili changamoto kubwa ni migogoro ya ardhi kati ya mamlaka husika na wananchi.
"Katika kikao hiki kitu kikubwa ninachotaka tujadili tunaondokaje kwenye migogoro ya ardhi kati ya serikali na wananchi kwani sehemu kubwa ya wananchi wanamanunguniko juu ya maeneo yao"kuongeza kusema iliyoombwa tijitengenezee njia huyo Mbele tunapokwenda lazima tuondoe migogoro ya ardhi kwa wananchi wetu na ndio maana nilipofika tu Dodoma tulianzisha kampeni iliyojulikana kama ziro migogoro ambapo zaidi ya migogoro 300 iliorodheshwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde ameitaka idara ya migogoro ardhi jiji iongeze ufanyaji kazi vizuri na iangalie namna nzuri ya kuona kero za migogoro ya ardhi zinaisha.
" Idara ya ardhi fanyeni kazi kwa kumuhofia Mungu na kuzihofia nafsi zenu kwani manungu'niko ni mengi katika eneo la ardhi boresheni huduma zenu,"amesema Mavunde.
Naye Mstahiki Meya wa Dodoma Devis Mwamfupe amesema fedha hizo waliomba kwa utaratibu na zilipitishwa kwenye kikao cha baraza la madiwani hivyo ni vyema wangekaa na kulizungumza kwa utaratibu kuliko kulipaza.
Toa Maoni Yako:
0 comments: