"Ngoma Africa Band ya Ujerumani wameipigia saluti na kuitaja Golden speech"
Na mwandishi wetu Zainabu Ally Khamis
Hotuba ya Rais Mheshimiwa mama Samia Suluhu Hassan wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya alhamisi 22 April 2021 alipokuwa analihutubia Bunge la 12 mjini Dodoma, hotuba ya Rais imewavutia Wanatanzania wengi waishio ughaibuni au nje ya Tanzania.
Hotuba ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan imepokelewa kwa mikono miwili na kuonyesha mwangaza kwa Watanzania walio nje hususani katika masuaala ya kuwekeza nyumbani, alikaliliwa kiongozi wa kundi la muziki la Ngoma Africa Band Bwana Ebrahim Makunja a.k.a Kamanda Ras Makunja yenye makao yake nchini Ujerumani.
Mwanamuziki Ras Makunja alisema hotuba ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan tulikuwa tunaisikiliza mubashara (LIVE) ni hotuba tunayoifananisha na mwangaza mkubwa wa tochi au kurunzi unaotuonyeshea njia wapi tuelekee katika kujiimalisha kiuchumi na kijamii katika sekta zote kuanzia Kilimo, Elimu, Biashara, Uwekezaji, Viwanda, Utamaduni na Sanaa.
Hotuba ile ni dira ya muelekeo wa kuleta maana kamili ya furaha ya maisha kwa Watanzania, na ni wajibu wetu Watanzania wote wa ndani na nje kushiriki kuyatekeleza kwa vitendo yale aliyoyaeleza Mheshimiwa Rais katika hotuba yake Sisi Watanzania tunaishi nje tunasimama na kumuunga mkono", alimalizia kiongozi wa Ngoma Africa Band kamanda Ras Makunja kwa kusema Rais ni Imara "The Iron"
Utafiti wa masaa machache baada ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kulihutubia Bunge imeonyesha hotuba yake imewahamasisha wananchi wengi hadi jamii za kimataifa wakiwemo Watanzania waishio nje ambao mara nyingi wamekuwa wakipata usumbufu katika masuala ya kuwekeza nyumbani kutokana na usumbufu wa maofisini, wengi wao wanamisingi mikubwa na ya kati ambayo inaweza kuwekeza nyumbani na kuchangia pato la taifa na kuzalisha ajira kwa watanzania lakini wanakwamishwa sana na usumbufu wa maofisini mfano kwenye ofisi ya ardhi na upatikanaji wa leseni, wenzetu watanzania waishio nje mara nyingi wanajikuta wanapoteza muda mwingi kufuatilia mambo maofisini wajapo Tanzania na kujikuta kama wageni wakati Tanzania ni kwao.
Hotuba ya Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan imewavuta watanzania walio ughaibuni "GOLDEN SPEECH'
Toa Maoni Yako:
0 comments: