Mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha ABC Bible College and Training Center kilichopo jijini Dar es Salaam, Askofu Dkt.John Mwakilema Mkuu wa Chuo cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), (kulia mbele mwenye joho jekundu) akiongoza maandamano wakati wakiingia kanisani kuanza mahafali hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. Nyuma yake ni Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing Center (ABC) Flaston Ndabila na kushoto ni Askofu Mkuu James Mwaipyana wa Kanisa la Glory Temple Church International .
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John Mwakilema Mkuu wa Chuo cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akimkabidhi cheti Naomi Mushi mmoa wa wahimu wa masomo ya kuhudumia jamii hasa watu wanaokuwa katika majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko. Kushoto ni Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing Center (ABC) Flaston Ndabila.
Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing Center (ABC) Flaston Ndabila, akizungumza kwenye mahafali hayo.
Wakufunzi wa wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John Mwakilema Mkuu wa Chuo cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa ngazi ya Diploma ya Theolojia.
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
Wahitimu wa masomo ya Theolojia wakiingia kanisani kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa masomo ya kuhudumia jamii hasa watu wanaokuwa katika majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko wakiingia kanisani kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakiombewa.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John Mwakilema Mkuu wa Chuo cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akimkabidhi cheti, Dkt. Gad Ndabila.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John Mwakilema Mkuu wa Chuo cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akimkabidhi cheti Edward Mhoja mmoja wa wahitimu hao.
Na Dotto Mwaibale
CHUO cha ABC Bible College and Training Center kilichopo jijini Dar es Salaam kimefanya mahafali yake ya kwanza kwa kutoa wahitimu 20.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mahafali hayo Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing Center (ABC) Flaston Ndabila alisema kuwa Chuo hicho ni chuo kishiriki cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT)C
Alisema chuo hicho kinatoa Certificate na Diploma ya Theology na Certficate ya masomo ya kuhudumia jamii hasa watu wanaokuwa katika majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko na kuwaelimisha juu ya kanuni bora za afya yao yaani Community Health Worker kwa kushirikiana na Bright Fature Ministries (U.S.A)
"Chuo chetu kinatumia darasa lililopo katika kanisa letu hapa Mtaa wa Mandela Tabata wakati huu tukiendelea na ujenzi wa chuo kilichopo Manispaa ya Ilala eneo la Kinyerezi kwa Makofia."alisema Ndabila.
Ndabila alisema chuo hicho kina matawi katika Mkoa wa Morogoro ambacho kwenye mahafali hayo kimetoa wahitimu wawili na tawi la Kibaha ambao wametoa wahitimu watano na kuwa matawi hayo yanafundisha mwisho kiwango cha cheti.
Aidha Ndabila alisema kuwa masomo ya chuo hicho yalianza rasmi Novemba 5, 2019 na jumla ya wahitimu wakiwa ni 43, ngazi ya diploma wakihitimu 18, Community Health Worker wakiwa 20 na Certificate 7.
Ndabila alitumia nafasi hiyo kumshukuru Askofu Dkt.John Mwakilema Mkuu wa Chuo cha Zoe kwa kutoa mkono wa shirika na kutoa maelekezo maalumu ya somo la jinsi ya kuweka mikakati.
"Nitumie nafasi hii kuwashukuru walimu wote kwa muda wao wa kufundisha ambao ni Askofu Oreliani Ngonyani, Mchungaji Benjamin Mwalilino, Mwalimu Michael, walimu wa matawi ya Kibaha na Morogoro na Madam Tamari Shunda (U.S.A) kwa kuwesha darasa la Community Healthy Worker pamoja na Dkt. Barnabas (MD) na Dkt.Gad Ndabila (MD) kwa kufundisha vyema."alisema Ndabila.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo Askofu Dkt.John Mwakilema alisema kuwa nyakati hizi kuna umuhimu mkubwa kwa wachungaji kusoma na kuwa wabobevu wa masuala mbalimbali na si kujikita katika eneo moja tu la Theolojia jambo litakalo saidia kuleta mabadiliko chanya ya kiroho na maendeleo ya kiuchumi kwa waumini wao na kanisa kwa ujumla.
Katika mahafali hayo viongozi mbalimbali wa Serikali ya mtaa wa Mandela lilipo kanisa hilo waliudhuria wakiwepo Askofu Mkuu James Mwaipyana wa Kanisa la Glory Temple Church International, Askofu Sedrick Ndonde Katibu Mkuu wa Kanisa la Restoration Bible Church na Apostle John Kazidi wa Kanisa la Messiah Pentecoste Church ambao walikuwa wanenaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments: