Seif Shariff Hamad
Seif Shariff Hamad

KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amekiri hadharani kuwa amezeeka na kwamba yeye sasa ni Babu huku akimtaja Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi kuwa ni kijana mwenye nguvu. 

Akihutubia wafuasi wake katika Ofisi za ACT-Wazalendo, Vuga mara baada ya mapokezi ya wagombea wao, Seif Shariff Hama amesema “Pole Pole anasema kuwa mimi ni Babu, ati kizee! ni kweli nakubali kuwa mimi ni babu na wao mgombea wao Dkt. Hussein ni kijana, sasa nataka kuwauliza wajukuu zangu leo mtanichagua mimi babu au kijana?” Aliwauliza wafuasi wake ambao wengi walibaki na midomo wazi. 

Mgombea huyo wa Urais Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, katika hali ya kukata tamaa alieleza kuwa yeye akiwa Babu licha ya umri wake kuwa mkubwa lakini atamshinda Mgombea Kijana wa CCM jambo ambalo liliwafanya wafuasi wake kuanza kuguna chini kwa chini huku akiwatuliza kwa kuwataka wasiwe na wasi wasi na uzee wake. 

Ifikapo Oktoba mwaka huu, Babu Seif Shariff Hamad atakuwa na umri wa miaka 78. Itakumbukwa kuwa Seif Shariff Hamad ni mgombea pekee aliyegombea mara nyingi zaidi bila kushinda.

Alianza akiwa CCM Mwaka 1985 akashindwa na Sheikh Idriss –Abdulwakil, akaanza visa na vituko vya kuhujumu CCM ambapo Mwaka 1988 yeye na wenzake saba walifukuzwa Uanachama wa CCM. 

Mwana 1995 (uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi) aligombea na Dkt. Salmin Amour akashindwa. Mwaka 2000 aligombea na Amani Abeid Karume akashindwa. Mwaka 2005 aligombea tena na Karume akashindwa. Mwaka 2010 aligombea na Rais wa sasa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Maalim Seif akaangukia pua.

Mwaka 2015 Maalim Seif aligombea tena na kushindwa. Mwaka 2020 anagombea na kijana Dkt. Hussein Mwinyi, na CCM wana uhakika wa kumshinda 'asubuhi.' 

Hata mabango ya wafuasi wake pamoja na viongozi wenzake waliandika na kutamka maneno ya "Shikamoo Babu Seif"
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: